Kipa wa Real Madrid, Thibaut Courtois, ametangazwa rasmi kuwa mmoja wa wanahisa wapya wa klabu ya Le Mans inayoshiriki Ligue 2 nchini Ufaransa. Taarifa hiyo imetolewa na klabu hiyo Alhamisi, ikiweka wazi kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amejiunga na mradi mkubwa wa kuijenga Le Mans kuwa moja ya vilabu vikubwa nchini humo.

Courtois anaungana na mastaa wengine wa kimataifa kama gwiji wa tenisi Novak Djokovic pamoja na madereva wa Formula 1 Felipe Massa na Kevin Magnussen katika umiliki wa sehemu ya klabu hiyo. Hata hivyo, Courtois ndiye mchezaji wa kwanza wa soka kujiunga na kundi hilo la wawekezaji.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 33 amewekeza kupitia kampuni yake ya NxtPlay Capital, huku kundi la Kibrazil la OutField likikamilisha ununuzi wa hisa nyingi za klabu hiyo. Uongozi wa Le Mans umeeleza kuwa uzoefu wa Courtois kama mshindi wa UEFA Champions League mara mbili na bingwa wa La Liga utasaidia kuongeza thamani ya kiufundi na kibiashara ndani na nje ya uwanja.
Katika taarifa yao, Le Mans wamesema lengo kuu ni kuharakisha maendeleo ya miundombinu na kuimarisha msingi wa klabu kwa muda mrefu. Mradi mkubwa unaoendelea tayari ni ujenzi wa kituo cha mafunzo kitakacholenga kukuza vipaji vya vijana wa ndani, kwa matarajio ya kuifanya Le Mans kuwa kitovu cha maendeleo ya soka la vijana nchini Ufaransa.


