Tottenham Hotspur Women wamefuzu hatua ya robo fainali ya Women’s FA Cup kwa namna ya kipekee baada ya kuibuka na ushindi wa penalti 9-8 dhidi ya London City Lionesses kufuatia sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 120. Spurs waliokolewa na penalti ya dakika ya 95 kabla ya kuonyesha utulivu mkubwa kwenye mikwaju ya penati iliyokuwa na presha kubwa.
Spurs walianza kwa kasi na kupata bao la mapema kupitia Matilda Vinberg ndani ya dakika saba za mwanzo, akimalizia pasi safi ya Olivia Holdt. Wageni walitawala sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza, huku kipa Lize Kop akiokoa hatari ya wazi kutoka kwa Nikita Parris. Hata hivyo, mchezo ulibadilika ghafla mwanzoni mwa kipindi cha pili baada ya London City kusawazisha kupitia mabadiliko yaliyofanywa na benchi lao.
Luca Corrales na Danielle van de Donk walichangia bao la kusawazisha dakika ya 58, kabla ya Jana Fernandez kufunga bao la pili kwa shuti kali la mbali lililowaacha Spurs wakiwa nyuma kwa bao moja. Kadri muda ulivyokwenda, ilionekana Tottenham wako njiani kuondoshwa, wakishindwa kuvunja safu imara ya ulinzi ya wenyeji.
Hata hivyo, katika dakika ya tano ya nyongeza, Spurs walipata penalti baada ya mpira wa kichwa wa Bethany England kuzuiwa kwa mkono na Teyah Goldie akiwa kwenye mstari wa goli. Mwamuzi hakuwa na shaka kuashiria penalti, na England alifunga kwa utulivu kupeleka mchezo dakika 30 za ziada.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa




