De Reuck Akabidhiwa Dhamana Na Mashabiki Simba

Mlinzi wa kati raia wa Afrika Kusini, Rushayn De Reuck, ameendelea kuwa gumzo miongoni mwa mashabiki wa Simba SC kufuatia kiwango chake bora tangu ajiunge na klabu hiyo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Mamelod Sundowns ya Afrika kusini.

Jina la Rushine De Reuck halikauki kwenye vinywa vya Wadau wa michezo na Wanasimba, ambao wamekipokea kiwango chake kwa mikono miwili na kumkabidhi dhamana nzito ya kuiongoza safu ya ulinzi ya timu hiyo. Beki huyo ameonyesha uimara, nidhamu na uwezo mkubwa wa kusoma mchezo, hali iliyochangia kuimarika kwa ngome ya Simba katika mechi mbalimbali za mashindano ya ndani na kimataifa.

De Reuck Akabidhiwa Dhamana Na Mashabiki Simba

Kutokana na mchango wake mkubwa uwanjani na ushawishi ndani ya kikosi, kocha mkuu wa Simba, Steve Barker, aliamua kumpa kitambaa cha unahodha, akimkabidhi jukumu hilo lililokuwa likishikiliwa na mkongwe wa klabu hiyo, Shomari Kapombe.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Hatua hiyo imeonekana kuimarisha zaidi morali ya mchezaji huyo, ambaye ameendelea kuiongoza safu ya ulinzi kwa kujiamini, akihakikisha nembo ya Simba inalindwa kwa nguvu zote. Mashabiki wengi wanaamini kuwa uamuzi wa kumpa unahodha De Reuck umeleta utulivu na mshikamano mkubwa katika kikosi hicho Kwa kushirikina na walinzi wenzake wa klabu hiyo akina Wilson Nangu, Ismaila Toure na Vedastus Misinde kwenye eneo la ulinzi wakati.

De Reuck Akabidhiwa Dhamana Na Mashabiki Simba

Kwa sasa, De Reuck anatajwa kuwa moja ya usajili bora wa Simba msimu huu, huku akipewa sifa kwa mchango wake mkubwa ndani na nje ya uwanja. Wanasimba wana matumaini kuwa ataendelea kuiongoza timu hiyo katika mafanikio makubwa zaidi kadri msimu unavyoendelea.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.