Klabu ya Arsenal FC. imeibuka kinara katika hafla ya utoaji wa tuzo za London Football Awards 2026 zilizofanyika jana katika jiji la London, Uingereza, baada ya kujinyakulia tuzo kadhaa muhimu kutokana na mafanikio yao makubwa msimu huu.
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, alitangazwa kuwa Kocha Bora wa mwaka baada ya kuiongoza timu hiyo kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ikiwemo Premier League, huku mbinu na uongozi wake vikisifiwa kwa kuifanya timu hiyo kuwa miongoni mwa vinara wa soka jijini London.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Katika tuzo za wachezaji, kiungo wa Arsenal Declan Rice alitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Premier League kutoka klabu za London kutokana na kiwango chake bora msimu huu na mchango mkubwa katika safu ya kiungo ya timu hiyo.

Aidha, kipa wa Arsenal David Raya alitangazwa kuwa Golikipa Bora baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu langoni na kusaidia timu yake kupata matokeo chanya katika mashindano mbalimbali. Katika kipengele cha mchango kwa jamii, mchezaji wa Arsenal Eberechi Eze alitunukiwa tuzo ya Men’s Player in the Community Champion kutokana na juhudi zake katika kusaidia jamii kupitia miradi na shughuli mbalimbali za kijamii kupitia ‘THE EZE FOUNDATION’.
Kwa upande mwingine, klabu ya Chelsea FC nayo ilipata heshima katika hafla hiyo baada ya nyota wake chipukizi Estevao Willian kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora Kijana, akitambuliwa kwa kiwango chake bora na mchango wake ndani ya kikosi hicho.

