Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba SC Morice Abraham, amempongeza beki mwenzake Shomari Kapombe kwa nidhamu na kujituma kwake ndani na nje ya uwanja, akisema hayo ndiyo yamekuwa siri ya kudumu kwake kwa muda mrefu katika soka la ushindani nchini.

Morice Abraham, amesema Kapombe ni miongoni mwa wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu katika kikosi hicho, akieleza kuwa tabia yake njema na kujituma kwake kumemfanya kuwa mfano kwa wachezaji wengine ndani ya timu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Hata hivyo Morice amesema mbali na soka, Kapombe ana maisha yenye utaratibu mzuri kwani hanywi pombe, havuti sigara na pia huepuka sehemu zisizokuwa na umuhimu kwake, jambo linalomsaidia kuendelea kuwa na afya njema na uwezo mkubwa uwanjani.

Morice ameyasema hayo jana Ahamisi kwenye programu maalumu ya Simba ‘media tour’ iliyoa andaliwa na Bodi ya ligi TPLB kwa ajili ya wanahabari kuvitembelea vilabu vinavyo shiriki ligi kuu na kufanya navyo mahojiano.

Aidha, Morice ameeleza kuwa Kapombe ni mtu wa ibada na hupenda kutumia muda wake mwingi akiwa na familia yake pindi anapokuwa hana majukumu ya timu, hali inayomsaidia kuwa na utulivu wa kisaikolojia na kuzingatia zaidi taaluma yake ya soka.

Kwa upande wa mazoezi, Morice amesema Kapombe ni miongoni mwa wachezaji wanaojituma zaidi ndani ya kikosi cha Simba licha ya kuwa na umri mkubwa ukilinganisha na baadhi ya wachezaji wengine, jambo linalowahamasisha vijana ndani ya timu kufanya kazi kwa bidii.

Kutokana na mchango wake mkubwa na historia yake ndani ya Simba, Kapombe anaheshimiwa sana na wachezaji wenzake ambao humchukulia kama kaka yao, huku mafanikio yake na uzoefu wake vikimfanya kuwa mmoja wa viongozi muhimu ndani ya kikosi hicho.


