Klabu ya Manchester United FC imeanza kuongeza kasi katika mchakato wa kutafuta kocha mpya wa kudumu, huku mustakabali wa kocha wa muda Michael Carrick ukiendelea kuwa haueleweki ndani ya klabu hiyo

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Baada ya mchezo wao dhidi ya AFC Bournemouth uliopangwa kufanyika Machi 20, United haitacheza tena hadi Aprili 13, kipindi ambacho kinatajwa kuwa muda muhimu kwa viongozi wa klabu kuanza majadiliano ya kina kuhusu makocha wanaoweza kuinoa timu hiyo.

Ripoti zinaeleza kuwa kocha wa timu ya taifa ya Germany, Julian Nagelsmann, ni miongoni mwa majina yanayowavutia viongozi wa Manchester United, huku klabu ikitarajiwa kufanya mawasiliano ya awali ili kujua kama angekuwa tayari kujiunga na timu hiyo siku zijazo.

Kocha mwingine anayefikiriwa ni Roberto De Zerbi ambaye kwa sasa hana timu, ingawa United haijakata tamaa ya kuwafuatilia hata makocha ambao tayari wanafanya kazi katika vilabu au timu nyingine endapo wataona kuna nafasi ya kuwapata.

Licha ya Carrick kufanya kazi nzuri hadi sasa na kuiweka United katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Premier League, uongozi wa klabu bado unaendelea kuchunguza chaguo mbalimbali kwa ajili ya mpango wa muda mrefu, hasa baada ya kichapo cha hivi karibuni dhidi ya Newcastle United FC kuonyesha kuwa timu hiyo bado inahitaji maboresho zaidi.

