Bodi ya ligi (TPLB) imetangaza rasmi mabadiliko ya uwanja kwa mchezo namba 30 wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Tanzania Prisons na Yanga sc uliopangwa kuchezwa Machi 12, 2026. Awali mchezo huo ulipangwa kufanyika katika uwanja wa Sokoine majira ya saa 10:00 alasiri.

Kwa mujibu wa taarifa ya TPLB, mchezo huo sasa utafanyika siku hiyohiyo lakini katika uwanja wa Jamhuri Dodoma kuanzia saa 2:00 usiku. Mabadiliko hayo yamefanywa kufuatia kufungwa kwa Uwanja wa Sokoine baada ya maelekezo kutoka Kamati ya Leseni za Klabu ya TFF.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Awali klabu ya Tanzania Prisons ilitoa taarifa kwa umma ikieleza kuwa kufungwa kwa uwanja wa Sokoine kungeifanya timu hiyo kucheza michezo yake ya nyumbani katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Tabora kwa muda, wakati ukarabati ukiendelea.

Hata hivyo, baada ya tathmini na maamuzi ya bodi ya ligi, imeamuliwa kuwa mchezo huo muhimu dhidi ya Yanga sc uhamishiwe katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma badala ya Tabora kama ilivyotangazwa awali na klabu ya Tanzania Prisons. Sababu ya mabadiliko hayo ni kufungwa rasmi kwa Uwanja wa Sokoine na Kamati ya Leseni za Klabu ya TFF, hatua iliyolazimisha wadau wa ligi kufanya marekebisho ya haraka ili kuhakikisha ratiba ya ligi inaendelea bila kuathiri ushindani wa mashindano hayo.

Bodi ya ligi TPLB imewataka wadau wote wa mchezo huo wakiwemo klabu shiriki, mashabiki na waandaaji wa maandalizi kuzingatia mabadiliko hayo mapya ya uwanja na muda wa mchezo ili kuhakikisha maandalizi yanaenda sawa kwa pambano hilo la Ligi Kuu Bara.

