Vilabu vya EPL Vyaanza Bila Ushindi Hatua ya 16 Bora UCL

Vilabu kutoka ligi kuu ya uingereza EPL vimeanza vibaya hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League baada ya kupata matokeo yasiyoridhisha katika michezo ya awali iliyochezwa Jumanne na Jumatano, huku kukiwa hakuna timu hata moja iliyofanikiwa kupata ushindi.

Vilabu vya EPL Vyanza Bila Ushindi Hatua ya 16 Bora UCL

Jumanne, wawakilishi wa EPL Liverpool FC walipata kipigo wakiwa ugenini baada ya kufungwa bao 1-0 na Galatasaray SK katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa. Matokeo hayo yanawaweka Liverpool katika nafasi ngumu kabla ya mchezo wa marudiano utakaochezwa nchini England.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika mchezo mwingine, wa timu kutoka EPL  Newcastle United walishindwa kutumia faida ya kucheza nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya mabao 1-1 dhidi ya FC Barcelona, matokeo yanayoacha kila timu ikiwa na nafasi sawa kuelekea mchezo wa pili.

Vilabu vya EPL Vyanza Bila Ushindi Hatua ya 16 Bora UCL

Kwa upande wa mwakilishi wa EPL Tottenham Hotspur, walipata kipigo kizito cha mabao 5-2 wakiwa ugenini dhidi ya Atlético Madrid, matokeo yaliyopunguza kwa kiasi kikubwa matumaini yao ya kusonga mbele hatua inayofuata ya mashindano hayo makubwa barani Ulaya.

Jumatano, hali haikuwa tofauti kwa Arsenal FC ambao walipata sare ya mabao 1-1 wakiwa ugenini dhidi ya Bayer Leverkusen. Sare hiyo inaacha pambano hilo likiwa wazi huku kila timu ikihitaji ushindi katika mchezo wa marudiano.

Vilabu vya EPL Vyanza Bila Ushindi Hatua ya 16 Bora UCL

Nayo Manchester City ilikubali kipigo kizito cha mabao 3-0 kutoka kwa Real Madrid CF, wakati Chelsea FC wakipokea kichapo kikubwa zaidi cha mabao 5-2 dhidi ya Paris Saint-Germain, hali inayozifanya timu za EPL kuingia katika michezo ya marudiano zikiwa chini ya presha kubwa ya kurekebisha matokeo hayo.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.