Klabu ya Simba SC imeanza safari kuelekea Arusha baada ya kucheza mchezo wake wa Ligi Kuu ya NBC jana dhidi ya Singida Big Stars katika Uwanja wa Singida na kufanikisha ushindi wa mabao 2-1.

Katika mchezo huo, mabao ya Simba yalifungwa na Anicet Ura na Elie Mpanzu, huku bao la Singida BS likifungwa na Ndumumwe Mossi. Ushindi huo umewaweka Simba katika hali nzuri huku wakijiandaa kwa mchezo mwingine unaofuata kuhakikisha wanasonga mbele katika Ligi Kuu ya NBC.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Huko Arusha, Simba inatarajia kucheza dhidi ya TRA United tarehe 14 Machi, 2026, ambapo wanajiandaa kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ili kudumisha nafasi yao kileleni mwa ligi.

