Kocha wa muda wa Manchester United, Michael Carrick, amesema anatarajia timu yake kuonyesha mwitikio mzuri watakapokutana na Aston Villa katika mchezo wa Premier League utakaochezwa katika Uwanja wa Old Trafford.

Manchester United inalenga kupata ushindi wa tano mfululizo nyumbani chini ya Carrick baada ya kupata mapumziko katikati ya wiki, wakati Aston Villa wao walikuwa wakicheza dhidi ya Lille OSC kwenye michuano ya UEFA Europa League. Tangu apewe jukumu la ukocha wa muda, Carrick ameshinda michezo sita kati ya nane na kuisaidia timu kupanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumzia kiwango cha kiungo wa Aston Villa Morgan Rogers, Carrick amesema anafurahi kumuona mchezaji huyo wa England akifanya vizuri chini ya kocha Unai Emery.
Carrick alisema kuwa anafurahia kuona Rogers akipiga hatua kubwa tangu alipojiunga na Aston Villa akitokea Middlesbrough FC, akisema maendeleo yake yanaonyesha jinsi alivyojituma na kuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Villa pamoja na timu ya taifa ya England.
Kocha huyo pia alikiri kuwa kukutana na Aston Villa ni mtihani muhimu kwa timu yake, hasa baada ya kupoteza mchezo wa ligi kwa mabao 2-1 dhidi ya Newcastle United kwenye Uwanja wa St James’ Park mapema mwezi huu.
Hata hivyo, Carrick amesema kikosi chake kimejifunza kutokana na matokeo hayo na kina ari kubwa ya kurejea katika kiwango bora, akisisitiza kuwa wanajiandaa kikamilifu kwa mchezo huo muhimu huku wakilenga kuimarisha nafasi yao katika mbio za kufuzu UEFA Champions League msimu ujao.

