Pigo kwa Chelsea: Kisa Jeraha la Misuli Reece James Kuwakosa PSG

Nahodha wa Chelsea, Reece James, ataukosa mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint-Germain baada ya kupata jeraha la misuli ya paja (hamstring), kocha Liam Rosenior amethibitisha.

Pigo kwa Chelsea: Kisa Jeraha la Misuli Reece James Kuwakosa PSGJames alipata jeraha hilo mwishoni mwa mchezo wa Ligi Kuu England ambapo Chelsea walifungwa 1-0 na Newcastle United, na hakushiriki mazoezi kuelekea mechi hiyo muhimu itakayopigwa Stamford Bridge. Chelsea wanahitaji kupindua matokeo ya kufungwa mabao 5-2 kwenye mchezo wa kwanza.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Rosenior alisema bado hawajajua ukubwa wa jeraha hilo, lakini alikiri linaweza kuwa kubwa kutokana na aina ya majeraha ya misuli ya paja, huku akisisitiza kuwa mchezaji huyo atafanyiwa vipimo zaidi ili kubaini hali yake kamili.

Pigo kwa Chelsea: Kisa Jeraha la Misuli Reece James Kuwakosa PSGMbali na James, Chelsea pia wanakabiliwa na mashaka ya uwepo wa beki Malo Gusto ambaye anaumwa, pamoja na kipa Filip Jorgensen anayesumbuliwa na maumivu ya nyonga.

Hata hivyo, klabu hiyo imepata ahueni baada ya winga Pedro Neto kuruhusiwa kucheza licha ya kupewa onyo na UEFA kufuatia tukio la kumsukuma mpira kijana wa kuokota mipira katika mchezo wa kwanza.

Pigo kwa Chelsea: Kisa Jeraha la Misuli Reece James Kuwakosa PSGPamoja na changamoto za majeraha, adhabu za nje ya uwanja pamoja na matokeo mabaya ya awali, Rosenior amesisitiza kuwa Chelsea bado wanaamini wanaweza kufanya vizuri dhidi ya PSG, akieleza kuwa kikosi, benchi la ufundi na mashabiki wanapaswa kuendelea kuamini hadi mwisho.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.