Van Dijk Aingia Hatarini Liverpool Kwa Hofu ya Kadi

Nahodha wa Liverpool, Virgil van Dijk, yupo kwenye presha kubwa ya kinidhamu wakati timu yake ikijiandaa kwa mechi muhimu ya marudiano ya hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League dhidi ya Galatasaray. Baada ya kupoteza 1-0 nchini Uturuki, Liverpool wanahitaji ushindi Anfield ili kusonga mbele, lakini kivuli cha adhabu ya kadi kinatishia mipango yao.

Van Dijk Aingia Hatarini Liverpool Kwa Hofu ya Kadi

Van Dijk sio peke yake aliye kwenye hatari hiyo, kwani pia Ryan Gravenberch na Curtis Jones wote wapo kwenye mstari mwembamba wa kusimamishwa. Wachezaji hawa tayari wana kadi mbili, na kadi moja tu ya njano kwenye mchezo huu itawafanya kuukosa mchezo ujao, ambao unaweza kuwa dhidi ya mabingwa watetezi Paris Saint-Germain.

Kwa mujibu wa kanuni za UEFA, mchezaji husimamishwa baada ya kufikisha kadi tatu za njano, na kadi hizo hazifutwi hadi robo fainali itakapokamilika. Hii inaongeza uzito wa mchezo wa leo, kwani sio tu ushindi unahitajika, bali pia nidhamu ya hali ya juu ili kuepuka kupoteza nyota muhimu.

Van Dijk Aingia Hatarini Liverpool Kwa Hofu ya Kadi

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Mbali na watatu hao, wachezaji wengine kama Dominik Szoboszlai, Alexis Mac Allister na Hugo Ekitike nao wapo kwenye tahadhari wakiwa na kadi moja kila mmoja. Hii inaifanya Liverpool kucheza kwa umakini mkubwa, kwani kila kadi inaweza kuwa na athari kubwa katika safari yao ya Ulaya.

Van Dijk Aingia Hatarini Liverpool Kwa Hofu ya Kadi

Kocha Arne Slot sasa anakabiliwa na kazi ngumu ya kusawazisha ushindani na nidhamu ya kikosi chake. Kwa Liverpool, UEFA Champions League ndio tumaini lao la mwisho la taji kubwa msimu huu, hivyo kupoteza mchezaji muhimu kama Van Dijk kwa sababu ya kadi kunaweza kuwa pigo kubwa sana katika ndoto yao ya ubingwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.