Mshambuliaji wa Manchester United, Joshua Zirkzee, anaripotiwa kuwa tayari amekubali kuondoka klabuni hapo majira ya kiangazi baada ya kushindwa kupata nafasi ya kudumu kikosini. Nyota huyo wa Uholanzi ameonekana kukata tamaa kufuatia kukosa muda wa kucheza, hali inayomfanya kutafuta mazingira mapya yatakayomrejea kwenye kiwango chake.

Zirkzee aliwasili Old Trafford akitokea Bologna FC akiwa na matarajio makubwa, lakini mambo hayajaenda kama ilivyotarajiwa. Mwaka 2026 umekuwa mgumu kwake, ambapo amecheza dakika 28 tu, huku kukosa hata nafasi ya kuanza mechi kukimfanya kupoteza imani na mustakabali wake ndani ya timu hiyo.
Hali ya sintofahamu ya makocha ndani ya Manchester United pia imeripotiwa kumuathiri kisaikolojia. Aidha, kukosa kucheza mara kwa mara kumemfanya kupoteza nafasi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi, jambo lililoongeza shinikizo kwake kutafuta mabadiliko mapema iwezekanavyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa sasa, wakala wake anaangalia uwezekano wa kumrejesha Serie A, ambapo aliwahi kung’ara. Juventus FC wanaonekana kuwa mbele katika mbio za kumsajili, wakimchukulia kama fursa ya gharama nafuu, huku wakipanga dili la mkopo lenye kipengele cha kununua moja kwa moja.

Mbali na Juventus, AS Roma pia wamewahi kuonyesha nia ya kumhitaji Zirkzee. Hata hivyo, mustakabali wake bado unategemea maamuzi ya Manchester United, lakini dalili zote zinaonyesha kuwa kuondoka kwake msimu huu wa joto ni jambo linalokaribia kutimia.

