Yanga SC Yatoa Onyo kwa Mashabiki Kufuatia Vitendo vya Kurusha Vitu Uwanjani

Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga SC Ali Kamwe, ametoa onyo kwa wanachama na mashabiki kufuatia vitendo vya kurusha chupa uwanjani katika mchezo wa ugenini dhidi ya Azam FC.

Yanga SC Yatoa Onyo kwa Mashabiki Kufuatia Vitendo vya Kurusha Vitu UwanjaniAkizungumza na waandishi wa Habari leo mach 20, amesema. “Nimeona ni vyema leo kuzungumza na Wanachama pamoja na Mashabiki wetu. Jana jioni, kupitia taarifa ya Bodi ya Ligi, sote tulishuhudia adhabu ya faini iliyotolewa kufuatia vitendo vya baadhi ya Wanachama na Mashabiki wetu kurusha chupa uwanjani katika mchezo wetu wa ugenini dhidi ya Azam FC.”

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Aliongeza kuwa: “Hii ni mara ya pili kwa Klabu yetu kutozwa faini ya aina hii. Ni muhimu kufahamu kuwa adhabu hizi zina athari kubwa kifedha na zikiendelea mwisho wake hautakuwa mzuri kwa maendeleo ya Klabu yetu.”

Yanga SC Yatoa Onyo kwa Mashabiki Kufuatia Vitendo vya Kurusha Vitu UwanjaniAli kamwe pia aliwaomba wanachama na mashabiki kudumisha ustaarabu wanapohudhuria michezo: “Napenda kuwaomba Wanachama na Mashabiki wetu wote kudumisha ustaarabu wanapofika uwanjani kuishangilia Klabu yetu. Furaha inapopatikana, tushangilie na pale ambapo kuna jambo halijaridhisha, tunaweza kuonesha hisia zetu kwa njia za amani kama vile kuzomea lakini si kwa kurusha chupa au vitu vingine hatarishi wala kusababisha fujo.”

Yanga SC Yatoa Onyo kwa Mashabiki Kufuatia Vitendo vya Kurusha Vitu UwanjaniAlisisitiza kuwa vitendo vya aina hiyo havina nafasi katika soka na si sehemu ya utamaduni wa klabu: “Vitendo vya namna hiyo havina nafasi katika soka letu na si sehemu ya utamaduni tunaotaka kuujenga. Tushirikiane kulinda taswira ya Klabu yetu na kuhakikisha mazingira ya uwanjani yanabaki kuwa salama, yenye heshima na yanayovutia kwa kila mmoja.”

Yanga SC Yatoa Onyo kwa Mashabiki Kufuatia Vitendo vya Kurusha Vitu UwanjaniKauli hiyo ni ishara ya Yanga SC kuhimiza mashabiki kushiriki kwa njia salama na kuhakikisha michezo inaendelea kwa heshima na amani, huku ikilinda hadhi na taswira ya klabu.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.