Beki wa Arsenal FC, William Saliba, ameondolewa rasmi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu. Uamuzi huo umefanyika saa 24 tu baada ya kucheza dakika zote 90 kwenye fainali ya Kombe la Carabao dhidi ya Manchester City, ambapo Arsenal walipoteza mchezo huo.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Ufaransa, Saliba anakabiliwa na maumivu yanayojirudia kwenye kifundo cha mguu wa kushoto, hali inayohitaji mapumziko ya angalau siku 10 pamoja na matibabu maalum. Hivyo basi, hataungana na kikosi cha kocha Didier Deschamps kitakachosafiri kuelekea Marekani kwa mechi za kirafiki.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kuondoka kwa Saliba kumefungua mlango kwa beki wa Crystal Palace, Maxence Lacroix, kuitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha wakubwa. Lacroix amekuwa na msimu mzuri, akionyesha kiwango thabiti na kuvutia macho ya benchi la ufundi la Ufaransa.
Saliba amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Ufaransa tangu alipocheza mechi yake ya kwanza mwaka 2022, akiwa tayari amecheza mechi 31. Hata hivyo, majeraha yamekuwa yakimkumba mara kwa mara na kuathiri mwendelezo wake kimataifa, jambo ambalo sasa linaendelea kumuweka nje ya kikosi katika kipindi muhimu.

Ufaransa wanatarajiwa kucheza mechi za kirafiki dhidi ya Brazil na Colombia nchini Marekani, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya FIFA World Cup 2026. Hii itakuwa nafasi muhimu kwa Lacroix kujithibitisha na kuwania nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha taifa.

