Beki wa Real Madrid, Antonio Rüdiger, amefunguka kuhusu hatari anayoiwakilisha Harry Kane kuelekea robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich. Rüdiger hana shaka juu ya ugumu wa kazi inayowasubiri, akitambua ubora mkubwa wa mshambuliaji huyo wa England ambaye ameendelea kuwatesa mabeki msimu huu.

Akizungumza na Kicker, alisifu uimara wa Bayern, akisema, “Sisi Real Madrid tunajua tutakutana na timu ya kiwango cha juu yenye ubora mkubwa. Kwa sasa, hakuna changamoto ngumu zaidi. Wapo katika kiwango bora kabisa Ulaya pamoja na Arsenal.”
Pambano la moja kwa moja kati ya Rüdiger na Kane ndilo linatarajiwa kuvuta hisia zaidi. Kane amekuwa na msimu wa kipekee tangu ajiunge na Bayern, na Rüdiger anatambua kuwa kumzuia haitakuwa kazi ya mchezaji mmoja bali juhudi za timu nzima.

Rüdiger aliendelea kumsifia Kane kwa kusema, “Kwangu, Kane yupo ndani ya washambuliaji watatu bora duniani. Ubora wake ni wa kiwango cha dunia. Njia pekee ya kumdhibiti ni kwa kushirikiana kama timu na hata hivyo si jambo rahisi ndani ya dakika 180.”
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Real Madrid walifika hatua hii baada ya kuiondoa Manchester City, ambapo Rüdiger alicheza nafasi muhimu kumzuia Erling Haaland. Sasa atalazimika kutumia mbinu tofauti dhidi ya Kane, ambaye si tu mfungaji bali pia anajua kushuka chini na kutengeneza nafasi kwa wenzake.

Mchezo wa kwanza utapigwa Aprili 7 katika dimba la Santiago Bernabéu, huku marudiano yakipangwa Aprili 15 Allianz Arena, Ujerumani. Madrid watahitaji matokeo mazuri nyumbani kabla ya safari ngumu ya ugenini wanapopigania tiketi ya nusu fainali.

