Manchester United Yapata Nafuu Katika Mbio za Kumsajili Baleba

Klabu ya Manchester United imepata mwanga wa matumaini katika harakati za kumsajili kiungo wa Brighton & Hove Albion, Carlos Baleba, baada ya taarifa kuibuka kuwa thamani yake imeshuka ukilinganisha na msimu uliopita.

Manchester United Yapata Nafuu Katika Mbio za Kumsajili BalebaBaleba, mwenye umri wa miaka 22, awali alikuwa akitajwa kuwa na thamani ya zaidi ya Pauni milioni 100, lakini kwa sasa anaweza kupatikana kwa dau la kati ya Pauni milioni 70 hadi 85 kutokana na kushuka kwa kiwango chake msimu huu.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Kwa mujibu wa ripoti, Manchester United inamuona Baleba kama mrithi sahihi wa Casemiro katika nafasi ya kiungo mkabaji, hasa ikizingatiwa uwezekano wa nyota huyo kuondoka katika klabu hiyo katika dirisha lijalo la usajili.

Manchester United Yapata Nafuu Katika Mbio za Kumsajili BalebaChanzo cha karibu na klabu kilinukuliwa kikisema, “Baleba ana sifa zote ambazo United wanazitafuta nguvu, kasi na uwezo wa kuzuia mashambulizi pamoja na kuanzisha mipango ya ushambuliaji kwa haraka.”

Aidha, inadaiwa kuwa mchezaji huyo tayari ameafikiana masuala binafsi na Manchester United na anaonesha nia kubwa ya kujiunga na klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford.

Manchester United Yapata Nafuu Katika Mbio za Kumsajili BalebaHata hivyo, United itakumbana na ushindani mkali kutoka kwa Manchester City na Bayern Munich ambazo pia zinafuatilia kwa karibu maendeleo ya kiungo huyo wa kimataifa wa Cameroon.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.