Nyota Senegal Kusherehekea Tena Taji la AFCON Ufaransa

Mvutano wa taji la AFCON 2025 umeendelea kupamba moto huku timu ya taifa ya Senegal ikionyesha msimamo wake wazi kabla ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya  Peru.

Nyota Senegal Kusherehekea Tena Taji la AFCON Ufaransa Kuelekea mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa Stade de France, Senegal imeweka bango lenye nyota mbili kwenye eneo la benchi la ufundi na njia ya kutokea wachezaji (tunnel), hatua inayotafsiriwa kama ishara ya kujitangaza kuwa mabingwa wa mara mbili.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Hatua hiyo imekuja katikati ya mvutano unaoendelea na CAF kuhusu uhalali wa mataji hayo, jambo ambalo limeibua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau wa soka barani Afrika.

Nyota Senegal Kusherehekea Tena Taji la AFCON Ufaransa Chanzo kutoka ndani ya timu Senegal kilinukuliwa kikisema, “Hii ni njia yetu ya kuonyesha tunachokiamini. Tunaamini sisi ni mabingwa na tutasimama na hilo.” Kauli hiyo inaonyesha dhamira ya Senegal kusimamia msimamo wao licha ya utata uliopo.

Wachezaji, benchi la ufundi pamoja na mashabiki  wa Senegal wanatarajia kufanya sherehe za ubingwa ndani ya uwanja huo, wakilenga kuonyesha umoja na kuondoa sintofahamu iliyotokana na mzozo huo.

Nyota Senegal Kusherehekea Tena Taji la AFCON Ufaransa Mchezo kati ya Senegal na Peru unatarajiwa kuchezwa leo Jumamosi, Machi 28, 2026 majira ya saa 11:00 jioni kwa saa za Tanzania, huku ukiwa si tu mtihani wa kirafiki bali pia jukwaa la Senegal kuonyesha nguvu na msimamo wao mbele ya dunia.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.