Bruno Fernandez Aweka Msimamo Mkali ‘’Nahitaji Mataji Siyo Maneno’’

Nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, ameweka wazi mustakabali wake ndani ya klabu hiyo kwa kusisitiza kuwa anachotaka zaidi ni mafanikio ya timu na si ahadi zisizo na matokeo. Kiungo huyo ameeleza kuwa kiu yake kubwa ni kushinda mataji, akionya kuwa bila ushindani wa kweli, ndoto hiyo haiwezi kutimia.

Bruno Fernandez Aweka Msimamo Mkali ‘’Nahitaji Mataji Siyo Mneno’’“Nahitaji ushindani wa kweli ndani ya timu. Bila hilo, hakuna nafasi ya kushinda mataji,” alinukuliwa akisema Bruno, akionesha wazi kuwa matarajio yake ni kuona Old Trafford ikirejea kwenye enzi za mafanikio.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Licha ya kuwa nguzo muhimu tangu alipojiunga mwaka 2020, Bruno hajaficha ukweli kwamba anaweza kufikiria upya mustakabali wake iwapo timu haitabadilika kimtazamo na kimatokeo. Kauli yake imezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki na wachambuzi wa soka Ulaya.

Bruno Fernandez Aweka Msimamo Mkali ‘’Nahitaji Mataji Siyo Mneno’’Katika hali ya kushangaza, Bruno alifichua kuwa aliwahi kukataa ofa nono kutoka Al Hilal, ambayo ilimuwekea mezani mshahara wa pauni 700,000 kwa wiki. “Ilikuwa ni ofa kubwa sana, lakini nilichagua kubaki kwa sababu ya malengo ya kisoka,” aliongeza.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa klabu kadhaa kubwa barani Ulaya zinafuatilia kwa karibu hali yake, huku kipengele cha kuvunja mkataba wake kinachokadiriwa kufikia pauni milioni 57 kikiwa kivutio kikubwa kwa wanaomtaka.

Bruno Fernandez Aweka Msimamo Mkali ‘’Nahitaji Mataji Siyo Mneno’’Msimu huu, Bruno ameendelea kuwa na mchango mkubwa kwa English Premier League, akifunga mabao 8 na kutoa asisti 17. Swali linalobaki sasa ni je, Manchester United wataweza kumshawishi kubaki kwa mafanikio ya uwanjani, au pesa pekee haitatosha kumzuia kuondoka?

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.