Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann, ameitaka timu yake kubeba kiwango bora walichoonyesha kipindi cha pili kuelekea mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya UEFA Champions League dhidi ya Arsenal.
Atletico walilazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza, ambapo Julian Alvarez alisawazisha kwa mkwaju wa penalti kipindi cha pili baada ya Viktor Gyokeres kufunga bao la kuongoza kwa Arsenal kipindi cha kwanza.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Licha ya Atletico kumiliki sehemu kubwa ya mchezo, walishindwa kutumia nafasi walizopata, hali inayowaacha na kazi ngumu ya kwenda kushinda katika dimba la Emirates Stadium ili kufuzu fainali.
“Utendaji wetu kipindi cha pili ulikuwa bora zaidi kwa kasi na presha tuliyoweka. Hiyo ndiyo njia ya kubaki kwenye ushindani. Itakuwa mechi nzuri sana kucheza, iwe nyumbani au ugenini, itakuwa ya kusisimua—hiyo ndiyo uzuri wa soka,” alisema Griezmann.
Aliongeza kuwa kufungwa mwishoni mwa kipindi cha kwanza kuliwaumiza, lakini walifanya mabadiliko ya kimkakati yaliyosaidia kubadilisha mchezo, huku mashabiki wao wakitoa sapoti kubwa.
“Kufungwa mwishoni mwa kipindi cha kwanza kunaumiza. Tulifanya marekebisho mawili au matatu ya kiufundi ili kuboresha presha na mfumo wetu, na hilo lilileta tofauti. Pia mashabiki walitusukuma sana,” alisisitiza.
Griezmann, ambaye alipiga mpira uliogonga mwamba dakika ya 63, amesema alipata nafasi kadhaa za kufunga lakini hakufanikiwa, akiahidi kufanya vizuri zaidi katika mchezo wa marudiano.

“Nilipata nafasi tatu wazi kipindi cha pili lakini sikufunga; nina uhakika nitafunga katika mechi ya marudiano. Ndoto yangu kubwa ni kufika fainali, nimejiandaa vizuri na nitakuwa tayaritunatumaini kufanikisha hilo,” alihitimisha.

