Carrick Aupa Uzito Mchezo wa Man United dhidi ya Liverpool

Kocha wa Manchester United, Michael Carrick amesema kuwa mchezo dhidi ya Liverpool unabaki kuwa wa kipekee licha ya timu hizo kutokuwa kwenye mbio za ubingwa wa Premier League msimu huu. Timu hizo mbili zenye mafanikio makubwa nchini England zinatarajiwa kukutana katika dimba la Old Trafford siku ya Jumapili.

Carrick Aupa Uzito Mchezo wa Man United dhidi ya LiverpoolCarrick alieleza kuwa mchezo huo ni miongoni mwa mechi anazozipenda zaidi kutokana na historia na ushindani uliopo kati ya klabu hizo mbili. “Bila shaka huu ni mmoja wa michezo ninayoipenda sana, ni mchezo wa kipekee. Kuna michezo mikubwa na ushindani mwingine, lakini huu uko juu kabisa,” alisema.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Alisisitiza kuwa historia, ushindani na hisia kali vinaufanya mchezo huo kuwa wa kipekee kwa mashabiki na wachezaji.
“Historia yake, matokeo ya nyuma, msisimko na burudani pamoja na hisia zinazohusika vinafanya huu kuwa mchezo maalum sana,” aliongeza Carrick.

Carrick Aupa Uzito Mchezo wa Man United dhidi ya LiverpoolKocha huyo wa zamani wa United alisema timu yake imepiga hatua kubwa tangu msimu uliopita walipomaliza nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi, pointi 42 nyuma ya mabingwa Liverpool.
“Hii inaonyesha maendeleo ya kikosi chetu na namna tunavyozidi kuwa imara. Tunaingia kwenye mchezo huu tukiwa katika nafasi nzuri na matokeo mazuri,” alisema.

Carrick Aupa Uzito Mchezo wa Man United dhidi ya LiverpoolCarrick pia alieleza kuwa licha ya tofauti ndogo ya pointi kati ya timu hizo kwenye msimamo wa ligi, hawazingatii sana hilo kabla ya mchezo huo. “Tunatambua hali ya ligi na jinsi ilivyo karibu, lakini huu ni mchezo wa kipekee, hatuuchukulii kama mingine,” alifafanua.

Carrick Aupa Uzito Mchezo wa Man United dhidi ya LiverpoolAidha, Carrick alifurahishwa na kiungo Kobbie Mainoo kusaini mkataba mpya wa miaka mitano, akieleza kuwa ana mchango mkubwa katika kikosi. “Amefanya vizuri sana na bado ana mengi ya kuonyesha. Ni kijana mdogo lakini yuko kwenye kiwango kizuri kwa sasa,” alihitimisha.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.