Baada ya aliyekuwa meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane kurejea tena klabuni hapo, Real Madrid wanaripotiwa kuwa wamekubaliana kumsajili nyota mbrazili anayecheza nafasi ya ulinzi Eder Miltao kutoka Porto mwisho wa msimu huu.
Miltao ambaye ana umri wa miaka 21, alijiunga na Porto akitokea Sao Paulo mwaka 2018 na ameonekana kufanya poa kwenye Primeira Liga na Champions League.

Makubaliano ya Real Madrid yanatajwa kufanikisha mkataba wa mika 6 na dau sharti la kumnunua la paundi milioni 50. Nyota huyu anatajwa kuwa na uwezo wa kucheza nafasi ya ulinzi upande wa kulia na pia ana uwezo wa kucheza kama kiungo pale inapohitajika.
Staa huyu atakuwa ni mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Real Madrid chini ya Zinedine Zidane kama meneja kwa mara yake ya pili klabuni hapo.


Edgar
Sawa nakubali mwanetu
Furahav
Yuko vizuri kijana.
Povel
Gud news