Fununu za Usajili

Kwa sasa ligi nyingi zipo kwenye hatua za mwisho kabisa kuhitimisha mizunguko yake katika ngazi zote za ndani ya ligi husika. Kukiwa katika hatua hiyo mara nyingi hupelekea klabu nyingi kutathmini na kuangalia wapi waliteleza ili waweze kupaziba mapema sana.

Pia, kipindi hiki huwa ni maalum kwa wachezaji kuangalia upya mikataba yao kama bado inawapa nafasi ya wao kuendelea kusalia katika klabu hizo au wanahitaji kuongezewa mishahara kusudi wasaini mikataba yenye maslahi pande zote mbili. Hakika huwa ni kipindi chenye nia ya kuongeza nguvu kwenye timu. Baadhi ya majina yaliyoanza kuvunja vichwa vya habari ni:

Leandro Trossard

Nyota huyo anayekipiga katika klabu anayochezea Mtanzania, Mbwana Samatta. KRC Genk ameanza kuwafanya Arsenal waangalie namna wanavyoweza kumnasa kinda huyo mwenye miaka 24 ambaye kiwango chake kimemfanya mtu wa pekee na anayehitajika kikosini hapo. Hadi sasa amecheka na nyavu mara 19 akiwa ametoa pasi za magoli nane, hii ni katika mashindano yote. Kama watakubaliana atawagharimu Arsenal kiasi cha €16m na hiyo ni biashara nzuri kabisa.

Cedric Soares

Mlinzi huyo wa klabu ya Southampton anayekipiga kwa mkopo katika klabu ya Inter Milan amekuwa nguzo kubwa sana katika kikosi hicho cha Inter na walitegemea kufanya naye kazi muda wote lakini maafikiano hayajafikiwa kwa yeye kusalia mitaa hiyo ya San Siro. Baada ya taarifa hizo yaliyoanza kujiri ni kwamba Wolves wameliangalia suala hilo na wanamtaka nyota huyo.

Max Kruse

Tottenham wanataka kuingia sokoni kupambana na Inter juu ya nafasi ya kumnasa nyota huyo anayekipiga Bundesliga kwenye klabu ya Werder Bremen. Spurs wanamvizia mchezaji huyo ikiwa kama sehemu ya kumsubirisha ili kuona kama Harry Kane bado atashawishika kutimka klabuni hapo. Na kama ikitokea basi nyota huyo atatafutwa ili aweze kutumika. Kama Kane akishawishika kuondoka hilo litakuwa ni aina ya pengo ambalo halitazibika haraka.

Hector Herrera na Alex Telles, klabu ya Atletico wapo kwenye msingi huo wa kuangalia namna wanavyoweza kuwapata wachezaji hao kutokana na kufanya biashara ya mchezaji wao mmoja hivyo wanahitaji kuingia sokoni kuangalia mchezaji atakayewafaa ili na wao wamsajili. Na wachezaji hao wawili wameingia kwenye ramani za kusakwa ili waweze kusaidia huduma hiyo muhimu.

2 Komentara

    Asante kwa taarifa meridianbet

    Jibu

    Taarifa njema

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.