Stan Kroenke atawapatia Arsenal pesa za kuwasaida katika kipindi hiki cha mlipuko wa Corona, baada ya wachezaji kukubali kupunguzwa mishahara.
Kroenke amekuwa akikosolewa vikali na mashabiki wa Arsenal na ametuhumiwa kuwa hawekezi inavyotakiwa kwenye klabu.
Bilionea huyo amewahakikishia ataweka pesa kwenye klabu ili kusaidia masuala ya kiuchumi kipindi hiki msimu ukiwa umesimama.
Kroenke, ana utajiri wa $10 billioni (£8bn), pia anamiliki Los Angeles Rams kwenye NHL, wakati mkewe anamiliki Denver Nuggets kwenye NBA naColorado Avalanche kwenye NHL.
Wachezaji wa Arsenal wamekuwa kwenye mazungumzo na uongozi kujadili kuhusu kupunguzwa mishahara wakati msimu ukiwa umesimama.
Mikel Arteta ameripotiwa kuzungumza na wachezaji ili kukubali kukatwa 12.5% kwenye miezi 12 ijayo japokuwa alisimia hizo zinategemea kama itafuzu Ligi ya Mabingwa.
Arsenal wanakaribia kufikia makubaliano hayo na wachezaji wake baada ya Arteta Kuingilia suala hilo.
Ripoti imesema wachezaji 14 wa kikosi cha kwanza walikuwa kinyume na muswada huo wa kuwakata wachezaji mishahara. Wachezaji walidai kutaka kuhakikishiwa kama pesa hiyo kweli itapewa kwa wafanyakazi ambao sio wachezaji.


isha
Ahsante sana kroenke kwa moyo mzuri
Povel
Habar njema