Tetesi za Usajili

Real Madrid wapo nafasi nzuri ya kumsaini straika wa Norway, Erling Braut Haaland, 19, kutoka Borussia Dortmund, lakini miamba hiyo ya Bundesliga hawapo tayari kumuuza hadi 2022.

Tottenham Hotspur wamemuomba kocha wao wa zamani Mauricio Pochettino kukubali kupunguza fidia yake ya £8.5m ili kusaidia klabu katika anguko la kiuchumi.

Manchester United wanaongoza katika mbio za kumsaini kinda kiungo wa Birmingham Jude Bellingham 16 ambae ana thamani ya £35m. Chelsea na Borussia Dortmund nao pia wanamfukuzia Bellingham.

Wakala wa Real Madrid na mshambuliaji wa Colombia, James Rodriguez, 28, amewasiliana na Manchester United kuhusu uwezekano wa kumsajili kipindi cha kiangazi.

James Rodriguez

Bayern Munich wanamatumaini ya kumsaini winga Manchester City, Leroy Sane, 24, kwa £61m kipindi cha kiangazi. Wanga huyo wakimataifa wa Ujerumani amebakiza miezi 12 katika mkataba wake na City.

Everton wanataka kumsaini straika wa Lazi Ciro Immobile, 30, ana wamemtoa chambo Moise Kean 20, kama dili la kubadilishana.

Liverpool wapo kwenye mazungumzo na kiungo wa Inter Milan na Croatia, Marcelo Brozovic, 27,ili kumnasa.

Barcelona wanamuhitaji kiungo wao wa Brazil, Philippe Coutinho kwa msimu ujao, amesema kocha Quique Setien. Countinho kwasasa yupo kwa mkopo Bayern Munich, anawaniwa na Chelsea na Tottenham.

Beki wa kulia wa Barcelona Nelsom Semedo ameanza mazungumzo na klabu yake kuhusu mkataba mpya. Mreno huyo anataka kuhakikishiwa anapatiwa muda mwingi wakucheza kabla hajasaini.

Wachezaji wa Arsenal wanakaribia kukatwa 12.5% kwa mwezi ili kusaidia kupambana na janga la Corona.

Amazon wanavutiwa kuwa wadhamini wakuu wa uwanja mpya wa Tottenham.  

Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Darren Fletcher amerejea klabuni kama balozi wa klabu, United wamethibitisha.

2 Komentara

    Habar njema sana 👍

    Jibu

    Habari nzuri

    Jibu

Acha ujumbe