Vilabu vya Ligi Kuu ya Uingereza wameendelea kuwa pamoja kwenye lengo la kumalizia msimu, lakini muswada wa kumaliza ifikapo June 30 haukujadiliwa kwenye mkutano wa Ijumaa.
Vilabu vyote vimewakilishwa kwa simu ya video, wakati ajenda kubwa ilikuwa ni namna ya kumaliza msimu.
EPL wamesema ligi haitaendelea kama serikali haijaona sawa kufanya hivyo.
Hakuna mwakilishi aliyetoa wazo la kumaliza msimu ifikapo Juni 30 na suala la kukatwa mishahara na usajili hayajazungumziwa.
Msemaji wa EPL: “Sote tunafahamu changamoto kubwa ni COVID-19 hasa tunawaza wale walioambukizwa na janga hili.

“Kama ilivyo kwa biashara zingine na viwanda, EPL na vilabu vyake wanajitahidi kufanya mipango mikubwa. Tunawashirikisha wadau, ikiwemo warusha matangazo, lakini lengo letu ni kuhakikisha ligi itarejea pale itakapokuwa salama kufanya hivyo na kusaidiwa na serikali
“Afya ya wachezaji, makocha, viongozi wa vilabu na mashabiki ni kipaumbele chetu na ligi itaendelea pale wataalamu wa afya wakiruhusu.

