Jabulani- Mpira Ulioacha Historia Afrika ya Kusini

Jabulani ni mpira uliotengenezwa rasmi kwa ajili ya mashindano ya kombe la Dunia lililo fanyika Afrika ya Kusini mwaka 2010. Mpira huo ulitengenezwa kwa kuzingatia mazingira ya aina zote na mpira huo kwa nnje umepewa ulaini uliomfaya mtu anaeuchezea mpira huo kuhisi raha katika mchezo wa mpira wa miguu.

Mpira huo ulitengenezwa kwa mfumo kama wa pembe tatu hivi lakini kwa muonekan wa kawaida unauona kama ni wa mviringo (Duara) , Jabulani angola ndio mpira wa kwanza kutengenezwa na Adidas kwa ajili ya mashindano ya mataifa ya Africa yaliyofanyika Angola mwaka 2009 ambapo uliundwa kwa rangi nakshi za njano ,nyekundu na nyeusi zikielezea rangi za bendera ya nchi muandaaji wa mashindano hayo.

Rangi ya Dhahabu ya mpira huo iliitwa Jo’bulani, na huo sasa ulitumika katika mashindano ya kombe la dunia yaliyofanyika nchini Afrika kusini na neno la Jo,bulani ni mbadala wa jiji maarufu nchini humo la Jo,Burg au Johannesburg, ambako mechi ya ufunguzi ilichezwa. Rangi hiyo ya Dhahabu kwanza ilionesha rangi ya kombe la dunia la Fifa lakini pia liligusa jina lingine la umaarufu la mji wa Johannesburg (THE CITY OF GOLD).

Mashindano hayo yalitazamwa na mashabiki laki moja ndani ya Afrika kusini pekee , huku ikitambulika kua mshindano hayo yalikua ni ya 19 tangu kuanzishwa kwake, Bahati hiyo ya kugombea nafasi ya kugombea kuwa mwenyeji wa mashindano ya kombe la dunia ilikua ya Afrika kusini kutokana na Uzabuni wa kuwa wenyeji kuiangukia afrika, na baadae tarehe 11 juni mpaka julai 11 Afrika ya kusini kupata bahati hiyo.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.