Alphonso Davies amecheza kwa kiwango cha juu akiwa na Bayern Munich, hiyo imetosha kabisa kusaini mkataba mpya na miamba hao hadi 2025, Klabu hiyo ya Bundesliga imetangaza leo Jumatatu.
Davies, ambaye alijiunga na Klabu ya Vancouver Whitecaps ya nyumbani kwao Canada mnamo 2016, alisajiliwa na miamba hao wa Ujerumani baada ya msimu wa 2018, Mpango huo unaripotiwa kuwa ni wa jumla ya dola milioni 22, ndio Pesa nyingi zaidi kusajiliwa Mchezaji kutoka MLS, ulidumu hadi uhamisho wa Miguel Almiron kutoka Atlanta United kwenda Newcastle United kuweka rekodi mpya.
Davies mwenye umri wa miaka 19 hivi Sasa, amecheza kwenye mechi 35 akiwa na mabao mawili na Assist saba tangu ajiunge na Bayern… Wakati wa wakati wake huko MLS, Davies alikuwa na mabao manane na Assist 12 katika mechi 65.

Akicheza Kama beki au winga wa kushoto, Davies anachukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji bora wanaochipukia kutoka CONCACAF, na amecheza mechi 17 kwa timu yake ya taifa, Canada. Mkataba wake wa awali na Bayern ulikuwa unafikia mwisho 2023.
“FC Bayern ni moja ya vilabu bora ulimwenguni, na kwangu ni ndoto imetimia kucheza hapa,” Davies alisema. “Nilihisi furaha tangu siku ya kwanza. Ninataka kushinda mataji mengi iwezekanavyo na Klabu hii. Mawazo ni kutaka kucheza wakati wote na kushinda kila kitu hapa.” Alifuunguka baada ya kumwaga wino


Furahav
Baki tu hapo tu.
Issa
Safi sana kwake