Mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane hatojiunga na Real Madrid msimu huu wa joto, Kwa mujibu wa ripoti ya Daily Mail.
Baada ya kufanya biashara hapo awali dhidi ya Spurs kwa kuwasajili Luka Modric mnamo 2012 na Gareth Bale mnamo 2013, Los Blancos hawana nia ya kujaribu na kupata huduma ya Kane msimu ujao.
Madrid, chini ya Zinedine Zidane wanaripotiwa kutofanya usajili ghali msimu huu wanapokuwa wakijiandaa kupata athari ya kifedha kufuatia Janga la Coronavirus.
Madrid kutomsajili Kane msimu huu wa joto kunafuta nafasi za Tottenham kukamilisha hesabu yao ya kupata pauni 200m kwa mchezaji huyo.

Lakini Sportsmail inaelewa Madrid haina nia ya kujiunga kwenye mbio za kumuwania Kane kwa sababu athari za kifedha kufuatia kusimamishwa kwa LaLiga kumewaacha wakipanga kufanya uhamisho wa majira ya joto wa bei ndogo.
Nyota huyo wa England anaonekana kubakia ndani ya Premier league.


Furahav
Wamuache tu.
Fatina mfingi
Asanteh kwa taarifa meridianbet