Chelsea Kumwania Waldschmidt

Chelsea watafungua mazungumzo na Freiburg juu ya mpango wa kumsajili mshambuliaji wao, Luca Waldschmidt, kulingana na ripoti huko Ujerumani.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 amefunga mabao sita katika mechi 16 kwa Klabu hiyo ya Ujerumani msimu huu, lakini msimu wake umekuwa ukikumbwa na majeraha kadhaa tangu Oktoba.

Luca Waldschmidt akishangalia moja ya magoli yake

Kwenye Mashindano ya Ulaya (UEFA EURO) ya chini ya miaka 21 msimu uliopita, Waldschmidt alimaliza kama mfungaji bora wa mashindano hayo akiwa na mabao saba, Waldschmidt baadaye alipewa nafasi katika kikosi cha wakubwa cha Ujerumani na sasa ameitumikia katika mechi tatu.

Kocha wa The Blues, Frank Lampard amekuwa akifuatilia maendeleo ya Waldschmidt na ana hamu ya kumsajili mshambuliaji huyo.

Ripoti hiyo inadai kwamba sasa Chelsea itajadili mpango wa kulipa pauni milioni 20 kwa Freiburg… Lampard alikuwa na hamu ya kusajili mshambuliaji mpya kwenye dirisha la uhamisho la Januari lakini Chelsea haikuweza kupata Mchezaji yeyote.

Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Edinson Cavani alikuwa mmoja wa malengo ya Lampard lakini nyota huyo wa Uruguay alipendelea kuhamia Atletico Madrid.

2 Komentara

    Itakuwa poa sana.

    Jibu

    Mmh poa sana

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.