Unamjua Thomas Langu Sweswe aliyecheza dakika 90 bila kugusa mpira akiwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini. Mzimbwabwe huyo aliyezaliwa Agosti 9 1981 katika mji wa Gweru uliyopo katikati ya nchini ya Zimbwabwe. Ni moja ya beki visiki walicheza kwa mafanikio wakiwa na Kaizer Chief ya kwa Madiba.
Sweswe alianza kucheza mpira mwaka 2001 akiwa na CAPS United iliyopo mji mkuu wa Zimbambwe, alicheza mechi 22 na kufunga goli 1. Mwaka 2002 alijiunga na Sporting Lions FC alicheza mechi 31 japo sio kwa mafanikio sana.
Akasajiliwa na Real United ya daraja la kwanza mwaka 2004 kisha akajiunga na Highlanders FC ya Bulawayo lakini kujiunga kwake kulionekana kama mkosi kwani hawakushinda taji lolote pamoja na msimu uliyopita kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika na kunyakuwa Ngao ya Jamii alicheza mechi 26 tu.
Akatua Manning Rangers ya Afrika Kusini 2004 alicheza mechi 11 kabla ya kurejea Zimbwabwe na Dynamos FC kwa msimu mmoja akahamia Mwana Afrika FC ambayo walifanikiwa kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho ambalo walitolewa na TP Mazembe. Akarejea Dynamos FC msimu huo walishika nafasi ya pili nyuma ya Monomotapa United pia walifika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika walitolewa na Cotonsport.
Sweswe akasajiliwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka 3, akiwa Kaizer ndipo alipotengeneza rekodi ya Dunia baada ya kucheza dakika 90 bila kugusa mpira. Mechi yake ya kwanza ilikuwa michuano wa MTN 8 ambapo walishinda 3-1 msimu huo walimaliza nafasi ya 3. Thomas alicheza mechi nyingi lakini moja ya mechi zilizompa jina ni ile ya ligi ambayo waliichapa Orlando Pirates 3-1 na Sweswe alikuwa mchezaji bora wa mechi.

Goli lake la kwanza akiwa na Chiefs alifunga dhidi ya Mamelodi 1-0 Disemba 4 2011.
Baada ya kukupiga Kaizer Chiefs kwa miaka 3, Bidvest Wits walichukua kwa mkataba wa miaka 2 akakutana na Tinashe mchezaji mwenzake waliokuwa pamoja Chiefs, akacheza michezo 28 bila goli. Msimu wa 2013-2014 alipewa kibali cha makazi, hivyo kutambulika kama mchezaji wa ndani japo hakucheza mechi yoyote rasmi kwani alikuwa na majeruhi.
Sweswe alichezea ZPC Kariba kabla ya kustaafu, alistaafu 2017 akiwa na miaka 35 nchini kwao Zimbabwe.


Furahav
Mmh mvivu.
Issa
Ni balaa