Paulo Dyabala- Mjukuu Anaependwa na Bibi Kizee wa Turin

Paulo Bruno Exequeil Dybala fundi mmoja kutoka Cordoba nchini Argentina pale kwao wanaamini yeye ni fundi kuliko mtu yoyote Argentina ukimtoa Diego Maradona, ukifika pale usiwape stori tofauti na Paulo. Mitaani kwao wanaishi na falsafa hiyo, Paulo mwenyewe anaishi na falsafa hiyo, ni kijana mmoja jeuri sana wala hana muda wa kumnyenyekea Nahodha Lionel Messi kama wengine.

Dyabala

Kiburi cha Paulo ni cha asili kabisa, Babu yake Boleslaw Dybala ni mzaliwa wa Poland kijiji cha Krasniow na alikimbia Ulaya kutokana na vita kuu ya pili ya dunia, miaka ya 1940 huku ndugu wengine wakielekea nchini Canada, bila shaka unawafahamu Wapoland walivyo, hawajali sana. Kutokana na kipaji cha hali ya juu alipewa jina ‘La Joya’ yani kitu cha thamani, mtoto flani mwili wa plastic, akili ya chuma na vision kubwa ya soka kama Fizikia ya Isaac Newton.

Wakati dirisha la usajili linapamba moto ilisemekana Real Madrid na Manchester United wapo tayari kumtoa Paulo pale Turin, wakati huo Sarri hakuwa na mpango na fundi huyo, majukwaa na mashabiki wakubwa wa Juventus walivurugwa, walichanganyikiwa, inakuaje La Joya anasepa.

Juventus inatambulika kama La Vecchia Segnora yani Kibibi Kizee, wanaamini wao ni klabu kongwe na Mama wa soka la Italia, hivyo Mwanaume yoyote anaekuja kwa Bibi kucheza apambane kwa hali na mali, asimsaliti Bibi kwenye shida na raha, Bibi (Juventus) anawapa penzi zuri tu waume zake, hataki kukimbiwa

Mashabiki walitumia kurasa za Twitter na mabango kumsihi Paulo asiondoke Turin, ‘A man never leaves a Lady Paulo’ ujumbe aliandikiwa Paulo kuwa Mwanaume siku zote hamkimbii mwanamke, Paulo alikubaliana na mashabiki kuwa haina haja ya kumkimbia Mwanamke

Asubuhi moja akaenda kwa Makamu wa Rais Pavel Nedved na kumwambia haondoki kwenda popote, akashuka mazoezini na kumwambia Kocha Sarri kuwa haendi popote anasalia Juventus, huyo ndie Mpoland mwenye uraia wa Argentina na Italia bwana.

2 Komentara

    Yupo sahihi kabisa

    Jibu

    Sio powa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.