Bodi inayosimamia mashindano ya klabu bingwwa ulaya imepanga kuendelea na mashindano hayo mwezi juni mwaka huu lakini kwa zile nchi zinazokabiliwa zaidi na Janga la Korona (Covid19) itawabidi kukatisha ligi zao. Mataifa yote 55 ambayo ni mwanachama wa UEFA yalikutanisha viongozi wao wa soka kwa njia ya video na hapo ndio yalipangwa namna ya kumaliza mashindano hayo.

Licha ya hivyo, kutokueleweka kwa ratiba hiyo kunafanya mipango hiyo kua mi gumu na kwa mara ya kwanza UEFA imekiri kua kuna baadhi ya nchi hazita maliza ligi zao kwa urahisi “Kumekua na mapendekezo magumu kidogo kuhusu kumaliza ligi na makombe ya nchi wanachama, ila kwa zile ambazo zinauangalizi maalumu zinamaliziwa kwa utaratibu tutakao wapa ili kuvipa fursa vilabu vyao kushiriki mashinano ya ulaya, kama ikitokea kuna ligi ilikatishwa” Uliandikwa hivyo waraka wa UEFA baada ya mkutano wao.

, UEFA- Mashindano Tutamaliza Kwa Uangalizi, Meridianbet
Raisi wa UEFA Bw. Caferin

Haija elezwa wazi hayo mashirikisho yaliyopewa ruhusa ya kukatisha ligi zao, watazikatisha kwa kufuata vigezo gani, Ingawa UEFA wenyewe wanataka shirikisho la nchi husika likikatisha ligi yake basi waje na sababu za kuridhisha juu ya kwanini wamekatisha msimu mapema.

Mpango uliopo ni kucheza mashindano ya mwaka 2020/21 kwa ratiba ile ile ya kawaida lakini sasa kwa kuvurugika kwa ratiba hii ya msimu zezi hilo halitawezekana kwa urahisi. lakini pia ni wazi kua UEFA wanataka kumaliza masindano ya klabu bingwa na yale ya yuropa ndani ya msimu huu wa mwaka huu na kumalizia hatua ya 16 bora.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa