Barcelona kuuza haki ya Jina la uwanja wa Nou Camp kwa mara ya kwanza, na pesa zote zitakwenda kusaidia mapambano dhidi ya janga la Virusi vya Corona.
Mabingwa wa LaLiga, Barcelona wanatafuta mdhamimi wa kununua haki za jina la uwanja wa Nou Camp kwa mwaka mmoja katika juhudi za kupata fedha kusaidia jamii katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.
Bodi ya utendaji ya Barcelona leo Jumanne imetoa taarifa kuwa klabu itatoa fedha zote zitakazopatikana kwa kuuza haki ya jina la uwanja kusaidia kupambana na janga COVID 19.

Nou Camp ndio uwanja mkubwa barani Ulaya ukiwa na viti zaidi ya 99,000, na Haujawahi kuwa na mdhamini tangu kufunguliwa kwake mwaka 1957.
Uwanja huo utaendeleza jina la ‘Nou Camp’ na jina la mdhamini litaanza kisha litafuta jina hilo.


Furahav
Vizuri