Raisi wa Juventus, Andrea Agnelli anadaiwa kuwa ndiye alisisitiza kubaki kwa golikipa Gianluigi Buffon ‘Gigi” pale Allianz Stadium.
“Tunataka uendelee kuwa mmoja wetu” -Andrea Agnelli
Golikipa huyu mwenye miaka 42 kwa sasa, alirejea Italia baada ya kuutumia msimu uliopita kule PSG na amejikuta akiingia kwenye rekodi nyingine baada ya kuongeza mkataba wake wa sasa wenye thamani ya paundi milioni 1.5 kwa mwaka.
Kufikia msimu ujao, Buffon atakuwa anatimiza miaka 26 ya kucheza soka la kulipwa, ataingia kwenye rekodi nyingine ya kuwa mmoja ya mchezaji waliotumikia soka la kulipwa kwa mda mrefu zaidi.
Kwa mujibu wa Gazzetta dello Sport, Buffon aliambiwa Agnelli kuwa asalie klabuni hapo.
Buffon anasema alimwambia Agnelli kama anaona kumbakiza klabuni hapo ni chaguo sahihi basi kwake hana shaka kusalia na anafurahi kuendelea kuwepo.
Buffon anaingia kwenye orodha hii ya wachgezaji wenye umri mkubwa zaidi kutumia Serie A.
1. Italo Rossi (Pro Patria, 1951) – Miaka 52
2. Marco Ballotta (Lazio, 2008) – Miaka 44
3. Francesco Antonioli (Cesena, 2012) –Miaka 42
4. Gianluigi Buffon (Juventus, 2019) –Miaka 41
5. Alberto Fontana (Palermo, 2008) – Miaka 41


Mariam mtandama
Safi
Furahav
Hongera buffon.
Neema juma
Safi sana
felister
good news