Kumbukumbu Pekee ya David Moyes United

Kila meneja anakuwa anakumbukwa kwa mchango wa mafanikio ya klabu ambayo anakuwa anaitumikia. Wakati badhi ya meneja wakifanikiwa zaidi, David Moyes aliacha kumbu kumbu ya aina yake klabuni Manchester United.

Bosi huyu wa zamani wa Everton, hakupata mafanikio akiwa Old Traford baada ya kujaribu kuchukua mikoba ya Sir Alex Ferguson, mikoba iliyoonekana kumzidi kwa uzito. Ilikuwa ni miezi migumu 10 kwa David Moyes kudumu Man United.

Bosi huyu anaweza kuwa ni mmoja wa mabosi ambao wameacha kumbu kumbu ya kipekee klabuni hapo, kwa bahati mbaya kumbu kumbu yake si nzuri kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake.

Baada ya Moyes kuondoka mwaka 2014, United wamepita mikononi mwa mameneja wawili kabla ya kufika kwa Ole Gunnar Solskjaer. Moyes alisaini mkataba wa miaka sita pale United baada ya kutoka Everton, kwa bahati mbaya hata msimu haukuisha kabla ya Moyes kusepa huku Ryan Giggs akiwekwa kama meneja wa mda kumalizia msimu.

Moja ya vitu vinavyokumbukwa kwake ni pamoja na taji pekee la Ngao ya Jamii ambalo lilipatikana katika kipindi chake baada ya kuwachapa 2-0 Wigan Athletic.

4 Komentara

    Kocha bora

    Jibu

    Kocha mzuri sana

    Jibu

    David mayoes atakumbukwa daima

    Jibu

    Moyes ulikua mzigo uliopewa ni timu ambayo ilikuwa na hadhi tofauti kwa levo ulizotokea huko everton

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.