Nahonda huyo wa Yanga SC, Pappy Tshishimbi amesema amejipanga tayari kushindana na yoyote katika nafasi yake kwenye kikosi.
Kumekuwa na taarifa kuwa Yanga inahusishwa na kiungo mkabaji wa Rwanda, Ally Niyonzima, na kama atasainiwa ataleta upinzani katika nafasi hiyo dhidi ya Tshishimbi.

Niyonzima inasadikiwa kuwa kwenye orodha ya wachezaji ambao kocha Luc Eymael ana wahitaji, na Tshishimbi amekiri yupo tayari kuchuana nae.
Tshishimbi amekuwa chaguo la kwanza kwenye kikosi cha wananchi pamoja na klabu kubadili makocha.
“Napenda ushindani, mara nyingi nashangaa watu kuogopa ushindani, lakini kwangu napenda kwasababu ushindani ndio njia pekee ya kuboresha kikosi.”
“Kukiwa na ushindani mkubwa kwenye timu, ndio wakati kikosi kinakuwa bora na bora zaidi. Kama Yanga watasajili kiungo mkabaji mwingine ni bora kwasababu ndio kitu natamani kuona.
“Anatakiwa atue mapema inavyowezekana, ili tuanze ushindani kwenye kwenye timu.”


Mwajuma
Bora wanawajagwani waongeze majembe mengine
Mwajuma
Jagwani kitawaka🔥
Samira
Ni kitu kizuri sana kujiamini
Neema Juma
Namkubaliii kinoma