Manchester United wako tayari kuongeza juhudi zao za kumnasa beki wa Inter Milan, Milan Skriniar baada ya Waitaliano hao kuthibitisha kuwa mchezaji huyo anaweza kuondoka msimu huu wa joto.
Lakini wanakabiliwa na upinzani kutoka Real Madrid, ambao pia wana hamu ya kumsajili Mslovakian huyo aliye kwenye kiwango cha juu huko Serie A, Madrid wanatafuta mrithi wa muda mrefu kwa Sergio Ramos.
Inter wanaripotiwa kutaka ada ya karibu pauni milioni 52.5, ingawa hakuna klabu ambayo imeonyesha nia ya kulipa zaidi ya pauni 40m. Manchester City pia wameangalia harakati za Skriniar na Barcelona pia wamehusishwa na mchezaji huyo. Lakini ni United na Real ambao ndio vinara kuwania saini yake.

Mkataba wake huko San Siro unaendelea hadi Juni 2023 baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka minne msimu uliopita, lakini Inter wameamua kupata pesa ikiwa wanaweza.
Skriniar, amecheza mara 31 kwa timu yake ya taifa Slovakia, alianza kuichezea Zilina ya nchini mwake kabla ya kujiunga na Sampdoria kwa ada ya pauni 4.5m mnamo Januari 2016.
Alikaa miezi 18 na Sampdoria kabla ya uhamisho wa pauni 30m kwenda Inter uliomfanya kuwa Mchezaji ghali zaidi kwa Kislovakia kwenye historia.


Frank Patrick
Madrid itamfaa zaidi ni beki flan mpambanaji sana
Ernest
Muda wake sasa kulamba dili mono.
Christopher
United kila mchezaji wanamtaka mwishon Zinaishia kuwa tetes tu
Povel
Haende popote kambi thanks meridian kwa update za kisport na burudani
Theckla
Kwa upande wangu Real Madrid hawajawahi kushindwa kumsajili mchezaji yeyote pindi wakimuhitaji skriniar ni beki mzuri sana
Gabriel
Mtazamo wngu man u wanahitaj bek maana wako vbaya upande wa nyuma
Hamidu
Kwa Madrid sawa.ramos huyo umri unakwenda ..Kama watamsajili atakuja kuwasaidia #meridianbettz
Hamidu
Kwa Madrid sawa .Kama watamsajili atakuja kuwasaidia #meridianbettz
mwakalosi
Hana thamani hiyo huyo beki
Emmy cleopa
Kwa madridi itamfaa sana ila meridian ahsante kwa taarifa #meridianbettz
Antony Luseno
Njoo united ukalipwe vizuri
Salma
Meridian mko vizur kwa taharifa
Ester mmakasa
Habari ni motomoto kila iitwapo leo ,meridianbet ndo habari ya mjini.
Lombo
meridianbet hamjawai kuboa
winfrida
united jitaidini mumnase skriniar itakuwa poa sana
Ester jackson
Popote kambi tu
isha
Alambe tuu hilo dili ni nono mno
Fatina mfingi
Makala nzur