Nani ameeleza uhusiano wake na Sir Alex Ferguson, na amekiri alikuwa akimuogopa kocha huyo wa Manchester United katika kipindi cha mwanzo akiwa Old Trafford.
Mchezaji wa zamani Ureno ambae alisajiliwa United na Sir Alex kutoka Sporting Lisbon mwaka 2007 kwa £23m, alifunga magoli 40 na assist 73 katika michezo 230 kwa kipindi chote cha miaka nane aliyokuwa Old Trafford.
Alisema: “Mwazoni, nilimuogopa sana, kama baba, ukifanya kosa.
“Lakini nilimuogopa hadi nilipojifunza kumuelewa na kuweza kujieleza vizuri.
“Kingereza changu hakikuwa sawa wakati huo ukilinganisha na sasa, na baada ya kukifahamu vizuri, alianza kunisikiliza.
“Na kutoka hapo, nilijifunza vingi kutoka kwa Sir Alex Ferguson. Nini alitaka kufanya, alikuwa nani na mahusiano yetu yalikuwa bora.”

“Alikuwa jirani yangu na tulitumia treni kwenda London,” Nani alisema.
“Mke wake au familia yake ilikuwa ikimuacha kituo cha treni kwahiyo wakati wa kurejea nyumbani hakuwa na dereva wakumrudisha kwahiyo alikuwa akitafuta mtu anayeishi nae karibu kupeleka.e.
“Kwahiyo nikasema, ‘Sawa boss, Nitakupeleka nyumbani. Lakini siku niliyompeleka nyumbani ilikuwa siku tulicheza mechi dhidi ya Fulham ugenini na nilikuwa benchi.
“Ferguson ni mtu aliyekuwa na uwezo wa kuongoza watu wenye sifa tofauti, umri tofauti na tabia tofauti.
“Tabia yangu wakati huo, nilikuwa mdogo na haikuwa rahisi, nafahamu hilo, nmejifunza vingi na alinibadilisha. Haya ndio maisha, lazima ujifunze.”


Gabriel
Good news 👍@# meridianBetTZ
Lombo
heshima n kitu kzur sana
Povel
Ni moja Kati ya makocha Bora waliomalzah kwa muda wao kwa mafanikio makubwa so ikiwah chn yake ni Kama baba mlezi thanks meridian bet tz#
felister
ahsanteni meridian bet kwa taarifa
Asia Abdy
Waooh inapendeza sana
Adelta
👍
Antony Luseno
Kwa mchezaji yeyote lazima uwe na heshima kwa kocha wako.
Kenani
Heshima kwanza
Furahav
Vzr
Ernest
Safi sana Nani, Hivyo ndivyo professional anatakiwa awe haswa kwa kocha wake.
Mwajuma
Inapendenda sana mchezaji kumuheshimu kocha wake
Ester mmakasa
Umefanya vizuri sana Nani kwa kuheshimu sir Alex kama baba kwako ,heshima ni siraha .
Emmy cleopa
Vizuri sana #meridianbettz
Theckla
Mwalimu ni km mzazi ukihitaji mafanikio katika Jambo lako ni lazima uwaheshimu watu hawa nakufata ushauri unaopewa
mwakalosi
We call him the boss fargie
Hamidu
Safi.angebaki man utd angekuja kuwa Kama cr7 #meridianbettz
frank patrick
Kocha bora kwangu wa kipindi chote nashabikia mpira akifuatiwa na Klopp
Shafii
Fagason alikua mkali Sana kwa wachezaji ote alikua anaishi nao Kama watoto wake
aisha
Heshima ni kitu kizuri sana hasa ukijielewa
Lydia Emmanuel Magoti
Heshima kwanza
Neema juma
Safi sana heshima inanguvu mno