Timo Werner Hazitaki Man United na Chelsea

Mchezaji mshambuliaji wa klabu ya soka ya RB Leipzig, Timo Werner anaripotiwa kuwa anataka kwenda kwa klabu ya soka ya Liverpool pekee kwa msimu huu wa majira ya kiangazi na atakataa ofa zozote zile kutoka kwa klabu za Manchester United pamoja na ile ya Chelsea.

Klabu hizo mbili za Premier League zinamuwania sana mchezaji huyo na zimehusishwa katika usajili wake ujao wakati wa dirisha la usajili utakapowadia. Pia, klabu za soka za Barcelona pamoja na Bayern Munich zinamsaka pia.

Hata hivyo, Liverpool wanaonekana kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuwa naye kwa kumsajili. Imesemekana kuwa mchezaji huyo anapenda sana kuvaa daruga za klabu hiyo ya pale Anfield na siyo vinginevyo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 akitaka kuhama basi anatakiwa kuhama kwa malipo ya ada ya kumuachia (uhamisho) ambayo ni takribani £54m kwenye mkataba wake wa sasa kwa klabu ya Leipzig, ingawa inaweza kushuka na ikafikia hadi thamani ya £36m majira yajayo ya kiangazi.

Mchezaji mshambuliaji wa klabu ya soka ya RB Leipzig, Timo Werner anaripotiwa kuwa anataka kwenda kwa klabu ya soka ya Liverpool pekee kwa msimu huu wa majira ya kiangazi na atakataa ofa zozote zile kutoka kwa klabu za Manchester United pamoja na ile ya Chelsea.

Ripoti za mapema wiki iliyopita zimedai kuwa Werner atakuwa tayari kutumia msimu wake mwingine akichezea klabu ya Leipzig ili tu aweze kuondoka kwenda kwa Liverpool ifikapo mwaka 2021, huku kukiwa na mipango ya uhamisho wa klabu ya The Reds iliyoathiriwa na uwepo wa janga la Corona.

Mpaka sasa Werner amefunga jumla ya mabao 27 na amesaidia upatikanaji wa mabao mengine 12 katika jumla ya mechi 37 katika mashindano yote msimu huu.

15 Komentara

    Timo ni mshambiliaji mzur sana akienda Liverpool atajulikana sana coz Liverpool Kuna kikosi kazi kizur sana # meridianbet

    Jibu

    Timo jeshhhh timoo mtu mbaya

    Jibu

    Thanks meridian kwa habar za Kimichezo na burudani

    Jibu

    karibu Liverpool Timo

    Jibu

    Timmo anajua

    Jibu

    Fundi wa burdani uwanjan

    Jibu

    Aende uko haujui mpira.

    Jibu

    Liverpool watakuwa wamepata bonge la mchezaji.

    Jibu

    Timmo yupo vizur sana #meridianbettz

    Jibu

    Kikosi cha ushambuliaji cha Liverpool kitakuwa cha hatari sana

    Jibu

    Let wait and see if he may rejection offer from those clubs

    Jibu

    Dogo anajua sana! Tusubil tuone!

    Jibu

    Wachezaji wanaojiamini hivi Klopp ndio anawapendaga na umri wake pia akienda Liverpool ataongeza kitu

    Jibu

    Hapaswi kuchagua timu maisha ya mpira ni popote pale

    Jibu

    Timo karibu sana liverpool

    Jibu

Acha ujumbe