Manchester City ilionekana kuwa kwenye mkondo sasa wa kushinda mechi hiyo baada ya bao la Kevin De Bruyne katikati ya kipindi cha pili kufuta bao la ufunguzi la Maxwel Cornet katika kipindi cha kwanza.
Moussa Dembele aliingia uwanjani kama mchezaji wa akiba na kufunga mabao mawili ya dakika za mwisho wakati Lyon ikisababisha mshangao mwingine wa Ligi ya Mabingwa, kwa kuiondoa Manchester City ya Pep Guardiola.

Kinyume na matarajio yote, timu iliyomaliza katika nafasi ya saba katika msimu wa kandanda la Ufaransa, na ambayo ilikuwa imecheza mechi mbili pekee za ushindani tangu mapema Machi, sasa itacheza katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Jumatano dhidi ya Bayern Munich.
Hiyo bila shaka ni hatua kubwa kwa timu hiyo ya Rudi Garcia na lakini pia hakuna aliyetarajia kuwa wangewaondoa Juventus katika duru ya mwisho, achia mbali kuwaondoa City katika hatua ya robo fainali.
“Bado tuko mashindanoni, kumaanisha kuwa tuna timu nzuri,” Mshambuliaji wa zamani wa Celtic Dembele aliiambia televisheni ya Ufaransa ya RMC Sport. “Tunazungumzia mechi moja baada ya nyingine, hatutajisahau. Tutajaribu kuwa tayari kuvaana na Bayern.
Timu hiyo ya Guardiola ilikuwa imepewa onyo na Lyon, kwa kushindwa nyumbani na kisha kutoka sare ugenini dhidi ya klabu hiyo ya Ufaransa katika Ligi ya Mabingwa msimu uliopita. Lakini hiyo ilikuwa karibu miaka miwili iliyopita na Lyon imepoteza wachezaji kadhaa muhimu tangu wakati huo.

Matokeo haya, siku moja baada ya Bayern kuibomoa Barcelona 8 – 2, ni mshtuko mkubwa na pigo kubwa kwa malengo ya City chini ya Guardiola.
Subira yao ya kushinda Kombe la Ulaya itaendelea, hii ikiwa ni mara ya tatu mfululizo kuondolewa katika robo fainali. “Hivyo ndivyo ilivyo. Labda siku moja tutaweza kupenya katika robo fainali. Hatujaweza kufanya hivyo sasa, na hawa vijana wazuri kweli, lakini tutajaribu tena katika siku za usoni.” Alisema Guardiola.
Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Basi fahamu kuwa kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.


aisha
Oky tuwape hongera lyon kwa ushindi lakini huo ndio mpira hakuna cha kushangaa
Sauda
Safi sana Lyon
Sadick
Wahenga walishasema kwamba mpira unadunda hivyo unaweza kudunda kuelekea upande wowote na ndivyo ilivyokuwa. Hongera Kocha Garcia kwa mbinu za ushindi#meridianbettz
Saupha mohamed
Hongera sana. Lyon
Sabrina
Hongera sana Lyon ingawaje man city walishambuliwa sana lakini mliwazidi triki katika kupachika magoli
Njiku
Walijitahidi sana Lyon walicheza kwa kujiami na kushamulia kwa kushtukiza walifanya poa sana walilinda goli lao na walifanikiwa kuwatoa city
Nasra
Man City walijiamini Sana hii mechi bila kujua Lyon amekuja kwa nidhamu ya kimchezo mwisho wa mechi mancity kajikuta kadondokea pua.
Mwajumah
Hongera sana lyon ila Man city walijiamini sana hii mechi bila kujua lyon wamekuja na kinizamu za michezo#Meridianbettz
Dorophina
Hongera Lyon kwa kutufungia midomo ya man city
Ester jackson
Pongezi sana kwa Lyon mmeonyesha ushujaa wenu mbele ya man city
Fatina mfingi
Pongezi Sana lyon
Ernest Kimeru
Daaah kweli mpira na maajabu yakee aisee
Lydia Emmanuel Magoti
Safii Lyon kwatua mlio fikia inapendeza sana
Mwanahamisi
Hongera sana Lyon
Zeiyana
Me naona man city walisahau shauku yao kubwa walitaka kukutana na Bayern Munch sa walichokipata hiyo hinaitwa usitukane mamba kabla hauja vuka mto
Samiah
Pongezi kwa Lyon
Caroline
Keep it up Lyon
felister
Lyon wamejua kutuchania mkeka jamaniii
Tatu
Pongezi kwake
julie
pongezi kwao
Shafii
Unbelievable mwisho wa mashindano tusije tukashangaa kombe kabeba ambaye hatukumdhania.
Issa
City waliingia kwa kujiamini sana ila kaunta atack walizotumia lyon ziliwanufaisha na kutoka kidedea
Furahav
Liyon ndio mabingwa msimu huu.
Janeflora malisa
Hngr zao
Devotha
Hongera sana Lyon ila hakuna aliyetegemea kama man city atatolewa na lyon
Hope mwaikuka
Na hii ndo tuanita mpira dk 90
Povel
Congrat Lyon Aibu kwa man city
Leonard
Mpira umetuonyesha maajabu yake
David Pere
Kinyume na matarajio yote, timu iliyomaliza katika nafasi ya saba katika msimu wa kandanda la Ufaransa, na ambayo ilikuwa imecheza mechi mbili pekee za ushindani tangu mapema Machi, sasa itacheza katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Jumatano dhidi ya Bayern Munich.
Latifa juma mohamed
Hiyo ndio the day of wonderfull football cz city walijiamin Sana walijua Lyon hawezi kupindua kumbe muda mwngn ht mtt anamzidi maarifa mkubwa.
farida ahmadi
Hongera Sana Lyon
warda
Nilijua tu hili Gemu atashinda Lyon#Meridianbettz
magdalena
UEFA ya ajabu sana yani timu kubwakubwa zote zimetolewa ni jambo la kuhuzunisha maana watu tulijiwekea mazoea
Neema
Hongera sana Lyon
Shan
Wadau wengi tulikua tuna amini man u ndiye bingwa wa haya mashindano.
Khadija
hongera sana lyon
Gabriel
Lyon walicheza mpira mzur sana tatizo la Manchester city walijiamin kupita kiasi
Salma ngende
Safi sana lyon
jullie
hongera zao