Bado naiwaza fainali ya world cup 2006, Pirlo wa usiku ule hakuwahi kuonekana kabla. Usiku mmoja wa kiume sana katikati ya dimba. Wafaransa walilala wanaiota miguu yake. Waitaliano walilala wamekumbatia picha yake. Alikuwa kila kitu kwao. Aliitoa Italy kwenye miguu ya Gattuso na kuifikisha kwa Luca Toni. Alilimeza dimba lililokuwa na Vierra na Makelele
Huyu ndiye Andrea Pirlo, kipindi anatoka Ac Millan kwenda Juventus Buffon alisema ” wakati Pirlo ananiambia anakuja Juve nilisema neno moja tu Mungu yupo, mchezaji wa kariba yake anakuja kwetu tena bure? Hamna cha zaidi ya kusema Mungu yupo.” Huyu ndiye Pirlo ambaye wahuni wa Turin walimuita “architect”. Alikuwa mbeba ramani wao pale Aliianz stadium.
Andre Pirlo
Pale Millan wanamuita “il professore”, kwa kindereko ni “the professor”. Mtaalam fulani wa kupiga pasi. Hajawahi kutokea binadamu kama yeye kwenye nyasi San Sirro. Angepiga pasi katikati ya watu sita alafu bado ikaenda kwa muhusika. Miguu yake ilikuwa na bikari, penseli, ruler na ufutio. Angetazama kulia alafu akaweka pasi kushoto.
Kipindi anajiunga na Ac Millan Ancelotti aliamini Pirlo ni, kiungo mkabaji anayehusika na ushambuliaji. Waitaliano walimuona Ancelotti kichaa, Ashakum si matusi. Unamchezesha vipi kiungo mkabaji huyu mtu ambaye hana nguvu miguuni? Waliuzoea mpira wa akina Demetrio Albertini na Roberto Donadoni. Walimuona Ancelotti mpumbavu, nilitangulia kusema Ashakum.

Wiki mbili tu walishampokea, wakasahau mpira wa kina Marco Tardeli, Pirlo aliwaaminisha kiungo mkabaji si lazima atumie nguvu. Kilichofuata ni stori tu, ndiyo huyu Pirlo tunayomzungumza mpaka leo.
Licha ya kutokuwa na kasi, nguvu na stamina atakumbukwa kwa uwezo wake kufanya kucheza kila pande akiwa dimbani. Atakumbukwa kwa uwezo wake wa kupiga free kick. Iwe ku’assist’ au kuupeleka mojamoja kambani, alikuwa mtu maalumu wa hizo kazi. Kumbuka ile free kick kwake kwenda kwa Maldini kwenye ile fainali ya UEFA 2005, ile ni miujiza.
Vitabu vya historia vinadai ni kati ya wapigaji pasi bora kuwahi kutokea kwenye historia ya mpira. Saint Andrea Pirlo, injini ya Millan.
Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.


Nasra
Pirlo alikuwa Moto wa kuotea mbali katika career yake ya mpira.
Ester jackson
Good news
Fatina mfingi
Alikuwa hatar
Njiku
Huyo ndio pirlo
Ernest Kimeru
Jamaa ni fundi kiukweli haipingiki
Lydia Emmanuel Magoti
Huyo ndio Pirlo alikuwa mtu Atari sana
Dorophina
Pirlo alikuwa kiboko enzi zake
Sabrina
Ni yeyeeee Andrea Pirlo ni yeyeee alikua moto sana ni balaa alikamatia soka ni mmoja kati ya wapigaji pass bora jina lake lipo katika historia ya mpira.
Mwanahamisi
Gud news
Zeiyana
Alivuma sana enzi zake pirlo akiwa dimbani sikuzote yeye alikua na kiu ya mpira tu
rama
Maoni:pirlo mtu atari sana huyo
Samiah
Gud
Caroline
Good boy
felister
ni yeye pirlo hana mpinzani uyu
Tatu
Ni yeye pirlo
Sadick
Hamu yangu kuona ufundi wake uwanjani anahamishia kwenye nafasi yake akiwa Kocha wa Juventus. Imeanza desturi ya timu kubwa kuchukua wachezaji wa zamani kuwa makocha wa Klabu walizochezea#meridianbettz
Shafii
Pirlo alikua Hana mfano akiwa dimbani mambo yake watu wameyamic Sana na penati zake za penenka style.
Mwajumah
Jamaa ni fundi sana #Meridianbettz
aisha
Pirlo alikua mwenye kipaji cha pekee lakini pia nidhamu na kujituma kwake ndio kulimfanya awe mwenye ubora wa kipekee enzi hizo
Issa
Pirlo master pass ni legend wa italia aliekuwa na kipaji matata
Furahav
Pirlo anajua.
Janeflora malisa
Nice
Devotha
Good
Hope mwaikuka
Pirlo mtu mbad
Povel
Pirlo natumain SOka bado linamdai kwny kaz ya Ukocha
Leonard
Pirlo fundi wa mpira
Latifa juma mohamed
Nice pirlo.
David Pere
Hamu yangu kuona ufundi wake uwanjani anahamishia kwenye nafasi yake akiwa Kocha wa Juventus. Imeanza desturi ya timu kubwa kuchukua wachezaji wa zamani kuwa makocha wa Klabu walizochezea
farida ahmadi
Habari nzuri Sana
warda
Pirlo anajua sana#Meridianbettz
Adelta
Good news @meridianbettz
Neema
Huyu ni yeye kabisaa pirlo alikuwa hatareee
magdalena
pirlo kipindi iko alikuwa anawika kwelikweli
Shan
Pirlo fundi wa mpira wadau wa mpira tunakumbuka sana zama zake.
Khadija
Good new
Gabriel
Pirlo alikuwa bonge la mchezaji wa kimataifa 👍
Salma ngende
Habari nzuri
Saupha mohamed
Habari njema
Theonestina
Asanteni kwa makala nzuri