De Gea Ajikingia Kifua

Kufuatia kuwa na msimu wenye maneno mengi kumuhusu kipa wa Manchester UnitedDavid De Gea, sasa ameamua kujikingia kifua na kuweka wazi lengo lake la kuipigania jezi namba 1.

Kwa misimu miwili iliyopita, De Gea anaonekana kushuka kiwango kwa kufanya makosa kadhaa ambayo yameigharimu timu kwa kiasi kikubwa. Inakumbukwa mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Chelsea, De Gea alifanya makosa mawili yaliyopekea kufungwa magoli mawili.

Wadau mbalimbali wa mchezo wa soka wamekuwa wakielezea hisia zao kuhusu kiwango cha De Gea,wengi wao wamekuwa wakimtaka Ole Gunnar Solskjaer kufanya maamuzi ya haraka na kumkabidhi mikoba kipa chipukizi Dean Henderson.

De Gea amenukuliwa akisema ” Ninajiamini, nimekuwa nikionesha ubora wangu kwa miaka mingi na hivyo muda wote ninapatikana kama kocha akinihitaji. Nipo tayari kucheza muda wowote na kuisaidia timu kama kawaida.”

Akizungumzia Mashindano ya Europa, De Gea amesema ” nadhani kiwango chetu kimeongezeka msimu huu. Tulikuwa tumezidiwa pointi 14 na timu iliyokuwa nafasi ya 3 kwenye Msimamo wa EPL lakini mwisho wa siku tumemaliza katika nafasi ya 3.

“Nadhani tumecheza vizuri kwenye michezo mingi. Kusema ukweli, tulistahili kucheza fainali. Pengine tulihitaji uzoefu zaidi kwenye kikosi na kutumia nafasi za kufunga tulizozipata. Tutaendelea kuongeza kiwango na kuipigania timu  pamoja na kushinda mataji msimu ujao.”

Baada ya kumaliza msimu kwa kutolewa kwenye nusu fainali ya Michuano ya Europa. Wachezaji wa Manchester United wamepatiwa likizo ya wiki 2 kabla hawajarudi tena kwenye mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao.


Drops and Wins!

Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.

Soma zaidi ucheze

38 Komentara

    De gea wasimulaumu bure wamlaumu kocha aliepanga kikosi cha wachezaji wabovu de gea yeye kazi yake ni kudaka tu na si uchezaji

    Jibu

    Nasemaje maneno maneno yao Man U yatawaponza ngoja tuu De Gea apate deal sehemu nyingine

    Jibu

    Makosa yapo hakuna mtu hasiyekosea. De gea amefanya makubwa sana kwenye clabu ya man u kwa likizo waliyo mpa naamni kabisa kuna mabadiliko makubwa sana tutayaona kutoka kwake

    Jibu

    Maoni:bado kiwango chake kipo vizuri sana

    Jibu

    De gea bado united inamhitaji

    Jibu

    Huo ndo mchezo ago maneno katika game kitu chakwaaida tu..

    Jibu

    De gea yuko vizuri ingawa kuna mambo yanajitokeza lakini sio kwa kusudi naninaamini kuwa ni kila bora zaidi kama watamuacha Chelsea watamchukua tena

    Jibu

    De gea kwa msimu miwili iliyopita anaonekana kushuka kiwango kufanya makosa kazaa ktk timu ingawa ni mchezaji anayejituma sana

    Jibu

    Bado anahitaji kuongeza ujuzi

    Jibu

    De gea yupo vizuri mbona na kiwango chake kipo vizuri

    Jibu

    Kwenye maisha kuna kupanda na kushuka

    Jibu

    Yupo kwenye kiwango kizuri sana

    Jibu

    mbona de gea ni kama anajihami hivi

    Jibu

    Msimlaumu De Gea usimamizi wakikosi kilikuwa sio poa nakwaujumla akuna kulaumiana nijambo lakulekebishwa

    Jibu

    De gea ni kipa mzuri na wana man u wanatarajia kua atakua clubuni hapo msimu ujao.

    Jibu

    Ila bado yupo vizuri

    Jibu

    Ni vizuri anajiamin

    Jibu

    Ila timu nzima ya man u inazingua hususan upande wa forward.. muache degea ajikingie kifua

    Jibu

    David de gea ni kipa mzuri Sana

    Jibu

    Lazima ajikubaliii ila asijebwetekaa

    Jibu

    De gea kiukwel msimu huu amezingua sana tuangalie Kama kwel ataweza kutetea jez namba 1 maana alipoangalia anapokonywa kabisa Henderson

    Jibu

    Ila bado yuko vizuri

    Jibu

    De Gea yupo vizur ni mchezaji mwenye kiwango chake

    Jibu

    Ni matokea tu ya mpira ila De Gea ni kipa mzuri tu

    Jibu

    aongeze juhudi

    Jibu

    Yuko vizur Sana

    Jibu

    Mi naamini de gea ni kipa bora Sana na katika soka kuna makosa madogo madogo ambayo yanatokea man u wakiruhusu kumuachia watakua wamepoteza jembe.

    Jibu

    Maisha ya de gea ndani ya United naona yamefika ukingon

    Jibu

    De Gea Inatosha Sasa tafuta timu nyingine tuachie Manchester yetu Dean Henderson arudi awe nambari moja

    Jibu

    Yupo vzr

    Jibu

    Yupo vzr

    Jibu

    Bado kiwango chake kipo vizuri sana # Meridianbettz

    Jibu

    Ila timu nzima ya man u inazingua hususan upande wa forward.. muache degea ajikingie kifua

    Jibu

    De Gea kutoka kuwa golikipa anayesifiwa hadi kujitetea , inawezekana ana tatizo jingine nje ya uwanja linaloathiri uwezo wake uwanjani#meridianbettz

    Jibu

    De gea ni goli kipa mzr sana ila kuna vitu kidogo vina hitaj marekebisho

    Jibu

    Kipa ninaemkubali sana

    Jibu

    De Gea bwana mie nisha mchoka

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.