Pierre-Emerick Aubameyang alifunga penalti ya ushindi na kuwaongoza Arsenal kunyanyua ubingwa wa Community Shield baada ya kuwaangusha Liverpool 5-4 kwenye mechi iliyowakutanisha ugani Wembley, Uingereza mnamo Agosti 29, 2020.
Mshindi wa mechi hiyo aliamuliwa kupitia penalti baada ya pande zote kuambulia sare ya 1-1 mwishoni mwa muda wa dakika 90.
Arsenal ndio waliokuwa wa kwanza kuliona lango la Liverpool kupitia goli la Aubameyang kunako dakika ya 12 kabla ya chipukizi Takumi Minamino kusawazishia Liverpool katika dakika ya 73.

Bao la Minamino ambalo lilikuwa lake la kwanza kambini mwa Liverpool, lilikuwa zao la ushirikiano mkubwa kati yake na mshambuliaji matata mzawa wa Misri, Mohamed Salah.
Ingawa Arsenal walilalamikia refa kwamba bao hilo lilifumwa wavuni na Minamino baada ya Salah kunawa mpira, teknolojia ya VAR ilibainisha vinginevyo.
Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa Liverpool kupoteza ubingwa wa Community Shield kupitia penalti. Mwanzoni mwa msimu wa 2019-20, Liverpool walizidiwa maarifa na Manchester City kwa mikwaju 5-4 ya penalti uwanjani Wembley.
Aubameyang alidhihirisha umuhimu wake kambini mwa Arsenal ambao kwa sasa wanatiwa makali na kocha Mikel Arteta.

Nyota huyo mzawa wa Gabon alifunga tena mabao mawili mnamo Agosti 1, 2020 na kusaidia Arsenal kuwabwaga Chelsea 2-1 ugani Wembley. Ushindi huo wa Arsenal uliwanyanyulia ubingwa wa Kombe la FA msimu huu wa 2019-20.
Ushirikiano mkubwa kati ya Aubameyang, Bukayo Saka na Ainsley Maitland-Niles ulitatiza pakubwa mabeki wa Liverpool ambao walishuhudia safu yao ya ulinzi ikivuja kupitia chipukizi Neco Williams.
Na baada ya kila kikosi kupiga jumla ya penalty nne, Aubameyang aliendea mkwaju wa mwisho kwa upande wa Arsenal na kumzidi maarifa kipa matata wa Liverpool, Alisson Becker.

Aubameyang anajivunia kufungia Arsenal jumla ya mabao 71 kutokana na mechi 110 zilizopita, na hakuna mwanasoka yeyote katika historia ya Arsenal amewahi kufunga zaidi ya idadi ya magoli matano ambayo yamefungwa na Aubameyang uwanjani Wembley.
Mnamo Agosti 28, Arteta alikiri kwamba Aubameyang alikuwa pua na mdomo kutia saini mkataba mpya kambini mwa Arsenal.
Baada ya kutia kapuni mataji mawili chini ya kipindi cha mwezi mmoja, Arsenal watakuwa wamefunga rasmi kampeni za msimu huu ambao ni wa kwanza chini ya Arteta.
Ingawa Liverpool walikosa huduma za beki Trent Alexander-Arnold na kiungo Jordan Henderson, kocha Jurgen Klopp aliwajibisha kikosi ambacho kilikuwa na wanasoka waliokuwa na uwezo wa kuwapepeta Arsenal ambao pia walikosa maarifa ya mafowadi Nicolas Pepe na Alexandre Lacazette.
Beti Mbio za Mbwa Mubashara
Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.


Latifa juma mohamed
Habari njema.
Povel
Hongera kwake Aubameyang🤝🤝🤝🤝
Agness
Asante kwa makala meridian
aisha
Kazi nzuri sana aliifanya aubameyang
Rehema Dickson
Asante kwa makala meridian
Antony Luseno
Arsenal walikuwa on fire hope msimu huu ni wao
Nasra
Kazi nzuri
Amiri Kayera
Mwanzo mzur wa msim
Rehema
Asante kwa makala mzur
neema hassan
Gud newz
farida ahmadi
Hongera Sana aubamayang
Caroline
Aubameyang yupo vizuri
Furahav
Aubameyang anatisha.
Rose kapinga
Hatari sana kijana,pongez kwake!!!
rama
pongezi kwake
Sadick
Aubameyang amedhihirisha kwamba aendelee kusalia Arsenal na kuipa mafanikio#meridianbettz
Fatina mfingi
Pongezi. Kwake
Hidaya
Asante meridianbet kwa makala hii
Tatu
Aubakeyang amefanya kazi nzuri
Saupha mohamed
Hongera yake
Mwanahamisi
Hatari sana pongezi kwake
Lydia Emmanuel Magoti
Ongera Sana Aubameyangu alinifurahisha Sana kupiga mkwaju wamwisho ndio ulio wanyanyua Arsenal
felister
pongezi kwake
Ernest
Aubameyang anawapa sana Raha Arsenal
Hope mwaikuka
Aubameyang katishaa sana
Amani
Safi sana mchezaji mzuri
JULIANA
Inapendeza
Mwajumah
Hongera kwake Aubameyang#Meridianbettz
Neema
Pongezi kwake Aubameyang
jullie
gud news
Dorophina
Hongera aubameyang endelea kupambana
kabogoro
auba anauwezo mkubwa sana akipata watu wa kumpa pas za mwisho.
Zeiyana
Aubameyang ndio Star pale arsenal kwa moto walianza nao arseno si wamchezo mchezo
Devotha
Hongera zake
lombo
vzr
Leonard
Aubemeyang yupo vizuri sana
Samiah
Safi
Edgar
Ongera arsenal
Asia Abdy
Anastahil pongez
Issa
Arteta ndoo ya kwanza
Aziza mushi
Amefanya kazi nzuri pongezi kwake.
Samira
Aubameyang jana ameoshenya yeye ni kiungo mzuri na bora wakati wote
Adelta
Yuko vizuri anastahili pongezi@meridianbettz
Janeflora malisa
Hngr zake
Ester jackson
Pongezi sana arsenal mana mmefanya kazi nzuri
Theckla
Aubameyang amejua kujitengenezea jina ndani arsenal
Theonestina
Hongera yake
Fatuma kasomo
Habari njema
warda
Hongera sana kwao#Meridianbettz
Sauda
Namkubali sana huyu jamaa
Johnmary joel
Namkubari na pongezi kwake#merdianbett
magdalena
uyu jamaa lile goli lake lilikuwa balaa sana
Salma ngende
Pongezi kwao
Tahiya
Tunatengemea mengi mazur kutoka kwake aubemayang
aisha
Auba ni moto anaipa the gunners matokeo muhimu katika mechi muhim
Omary lukumbi
Kazi mzur auba
Shani
Aubameyang fundi wa mpira.
Shafii
Pongezi kwa arsenal.
David Pere
Huu ni mwaka wa pili mfululizo kwa Liverpool kupoteza ubingwa wa Community Shield kupitia penalti. Mwanzoni mwa msimu wa 2019-20, Liverpool walizidiwa maarifa na Manchester City kwa mikwaju 5-4 ya penalti uwanjani Wembley.
Gabriel
Aubameyang amedhihirisha kwamba aendelee kusalia Arsenal na kuipa mafanikio