Kocha Ronald Koeman amesema fowadi Antoine Griezmann ndiye atasalia mwanasoka nguzo atakayetegemewa na Barcelona kadri kikosi hicho kinachojiandaa upya kwaajili ya msimu ujao.
Barcelona tayari wamefichua azma ya kuagana rasmi na mshambuliaji Luis Suarez huku wakitazamiwa pia kukatiza uhusiano na nahodha Lionel Messi anayehusishwa pakubwa na Manchester City, PSG na Inter Milan.
Suarez kwa upande wake anawaniwa pakubwa na Juventus na Atletico Madrid.

Kwa mujibu wa wakala Eric Olhats, Griezmann alikuwa tayari kuondoka Camp Nou mwishoni mwa msimu huu baada ya kulazimika kucheza katika nafasi ambayo hajaizoea kila mara alipowajibishwa kwa pamoja na Messi na Suarez katika klabu ya Barcelona.
“Alishiriki kikao na Koeman ambaye kwa sasa amemhakikishia kwamba atamchezesha katika nafasi inayomfaa zaidi uwanjani,” akasema Olhats.
Griezmann ambaye ni mzawa wa Ufaransa, alisajiliwa na Barcelona kutoka Atletico kwa kima cha Sh14 bilioni mwanzoni mwa msimu huu wa 2019-20.
Hata hivyo, hakuridhisha jinsi ilivyotarajiwa huku akichezeshwa kwa dakika zote 90 za mechi moja mara 19 pekee.
Chini ya wakufunzi Ernesto Valverde na Quique Setien waliopigwa kalamu na Barcelona msimu huu, Griezmann alifunga mabao 15 pekee kutokana na mechi 48.

“Alikuwa amefikia maamuzi ya kuagana na Barcelona hata kabla ya mechi ya robo-fainali ya UEFA iliyowashuhudia wakipigwa 8-2 na Bayern Munich.
Dalili zote ziliashiria kwamba hakuwa sehemu ya mipango ya klabu na hakuwa katika mawazo ya kocha. Hata hivyo, kwa sasa yuko radhi kusalia Camp Nou na Koeman atamuunga mkono kwa mengi,” akaongeza Olhats.
Kwa mujibu wa gazeti la L’Equipe, Griezmann kwa sasa atavaa jezi namba saba mgongoni badala ya 17 msimu ujao.
“Kwa heshima zote, Griezmann lazima arejee kucheza katika nafasi aliyozoea kutoka kwa waajiri wake wa zamani na timu ya taifa. Hapa ndipo msaada na ushauri wa kocha unahitajika zaidi,” akasema Koeman.
SHINDA NA HI LO
Sasa hii ni rahisi zaidi kupata USHINDI! Unatabiri karata ipi ipo chini au juu, kisha unakusanya mkwanja wako.


Adelta
Good news 👍
@meridianbettz
Mwajumah
Ni habari njema sana pale barca watakapo kuwa na luis suarez lkn inatupa mashaka kidogo Messi atakapotoka cjui kikosi kitakuaje#Meridianbettz
Gabriel
Hatimaye griezman anarejea Barcelona imekaa poa sana hii 👍
magdalena
griezmann ni mahili sana katika mpira na atafanya mambo makubwa sana barcelona
Caroline
Koeman kaongea ukweli
Dorophina
Hilo ndio tumaini lingine Barca alilobaki nalo ukimtoa Messi ataisaidia timu vizuri tu
Tatu
Griezmann anakuja kuziba pengo la mess
Ernest
Ni wakati wa Griezmann kuonyesha balaa lake sasa akiwa na Koeman
Mwanahamisi
Hatimaye griezman anarejea barcelona
lombo
habar njema
felister
hawa Barcelona wamekua kama wafa maji wanatapatapa tu
Rehema
Barcelona iko poa sana
Sauda
Arejea Barcelona na kuleta mafanikio makubwa.
Lydia Emmanuel Magoti
Griezmann anataka kuonesha mahajabu yake yupo vizuri
Nasra
Barcelona timu kubwa
Hilda
Jambo zuri
Fatina mfigi
Karibu barcelona
rama
sawa ndo chaguo la kocha
Shani
Habar njema
Sabrina
Barcelona ndio wajipange sasa
Johnmary joel
Sasa wajipange vizuri msimu huu ili wasirudi nyuma tena#meridianbett
Rehema Dickson
Good news 👍
Furahav
Koeman yuko sahii.
aisha
Ni kwer endapo mess atasep tutamuon grezman wa Atletico mweny njaa ya magor
Khadija
Barcelon chama la wana
Hidaya
Safi sana anaweza kulete mabadiliko mapya
Tatu
Barcelona wamepata jembe
Povel
Ngoj tuone
Saupha mohamed
Good news
Frank P
Barca walikuwa wanaenda kumpoteza Griezman thanx kwa Koeman kwa kutaka kumuibua tena tuombeee afanye na kwa dembele na coutinho
Fatuma kasomo
Habar njema
Amiri Kayera
Na mtabili km star ajaye pale barc endapo mess ataondok
Agness
Habari njema
Neema
Hakitaharibika kitu hapo. Akiwepo Griezmann mambo yatakuwaa fresh
Theonestina
Ni Jambo zuri sana
Rose kapinga
Afadhali labda Barcelona italudi kwenye ubora wake!!
Genia Sikaluzwe
Ni Jambo jema
Shafii
Na hii ndio sababu inayomfanya abakie barca licha ya kuhusishwa kurudi altetical.
Ester jackson
Dash back ishapotea tayari kawa wanataka Griezmann awe ngunzo imara itabidi watafutwe wachezaji wazuri wakumpa ushirikiano la sivyo ndiyo basii watabakia jina tu
farida ahmadi
Griezman ni mchezaji mzuri Sana pia hataisaidia Barcelona kwa kiwango kikubwa
Samiah
Nijambo jema
Hope mwaikuka
Ni kwel
Sadick
Griezman amehakikishiwa namba na alikuwa na hatihati ya kuondoka ndio maana amefurahia ujio wa Koeman ambaye gazeti moja liliwahi kumwelezea kama Trump wa Uholanzi#meridianbettz
warda
Sanaa