Kocha wa zamani wa Barcelona, Quique Setien na waliokuwa wasaidizi wake watatu wamefichua mpango wa kushtaki kikosi cha hicho kwa kutotii masharti ya kandarasi zao baada ya kufukuzwa mnamo Agosti 2020.
Kwa mujibu wa Setien na wenzake, Barcelona iliwapa notisi ya kukamilisha kandarasi zao mnamo Septemba 16 licha ya miamba hao wa soka duniani kuwatimua Agosti 17.
Aidha, Setien alisema kwamba hakuna yeyote katika benchi lake la ufundi pale Camp Nou alikuwa amelipwa fidia yoyote na barua ambayo yeye na wenzake walipewa na Barcelona mnamo Septemba 16 haikutaja mpango wowote wa kulipwa kwao.

“Barua kutoka kwa Barcelona inaashiria kwamba kikosi hicho hakina mpango wowote wa kutimiza masharti ya mikataba tuliyokuwa nayo tangu Januari 14, 2020,” akasema Setien.
Barcelona walimfuta kazi Setien siku tatu baada ya kikosi hicho kudhalilishwa kwa kichapo cha 8-2 kutoka kwa Bayern Munich ya Ujerumani kwenye robo-fainali za Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) jijini Lisbon, Ureno.
Kutimuliwa kwake kulimpisha mkufunzi Ronald Koeman aliyewahi kuvalia jezi za Barcelona kati ya 1989 na 1995. Koeman aliajiriwa baada ya kushawishika na kuacha kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi.
Setien ambaye pia amewahi kuinoa Real Betis, aliajiriwa na Barcelona mnamo Januari 2020 na alikuwa amesimamia jumla ya mechi 25 za Barcelona hadi kutimuliwa kwake.
Chini ya Setien, 61, Barcelona walikamilisha kampeni zao za msimu huu bila taji lolote kwa mara ya kwanza tangu 2008. Barcelona walikamilisha msimu huu kwenye La Liga katika nafasi ya pili kwa alama tano nyuma ya mabingwa Real Madrid.

Kichapo ambacho Barcelona walifungwa na Bayern kwenye UEFA kilikuwa cha nne katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ambayo iliwabandua kwenye robo-fainali za kipute hicho cha bara Ulaya.
Quique alimrithi kocha Ernesto Valverde uwanjani Camp Nou mwanzoni mwa 2020.
Baada ya kumtimua Setien, Barcelona walisema: “Haya ndiyo maamuzi ya kwanza kati ya mengi ambayo tunalenga kuchukua katika juhudi za kukisuka upya kikosi chetu.”
Barcelona pia walimtangaza Ramon Planes kuwa mkurugenzi mpya wa kiufundi kambini mwao. Planes alikuwa msaidizi wa Eric Abidal aliyetimuliwa na Barcelona akiwa mkurugenzi wa spoti.
SHINDA NA MERIDIANBET!
Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.


Caroline
Kama Barcelona hawakuwalipa hela zao.bc walikosea ilibidi walipwe stahiki zao
Dorophina
Haki yake setien kupata kile anachostahili kama wao klabu ndio waliovunja mkataba huo
Adelta
Wangelipana yote yasingekuwepo@meridianbettz
magdalena
mtu anabidi alipwe haki zake
Elika
Wangemalizana tu.sio poa kufika huko wanakotaka kufikishana
Ernest
Satien na wenzake wanahaki ya kudai fidia mbali na kuiongoza timu vibaya lakini mikataba inatakiwa izingatiwe
Rehema
Asante kwa taarifa
Sauda
Inabidi walipwe fidia
Shani
Itakua si fair play kwa Kufany hivyo
Antony Luseno
Endapo watashinda kesi watapiga mpunga mrefu
Mwajumah
Duuh atari iyo#Meridianbettz
Hopemwaikuka
Barca mpeni chake kama hamna issue nae
Hidaya
Sheria ifate mkondo wake
Lydia Emmanuel Magoti
Endapo watashinda kesi watapiga pesa ndefu
Zeiyana
Hapo sheria hifuate mkondo wake tu aki hitumike na kama ukijulikana ni kweli bac uwongozi utakua hupo mashakini
Angelina
Asante kwa makala
Sadick
Wakati Makocha wawili wa Yanga wanafikiria kuchukua hatua za kisheria kudai malipo yao kwa mara ya kwanza kwangu nasikia timu ya ulaya inashindwa kutimiza jukumu la kimkataba kwa waajiriwa wao wa zamani#meridianbettz
Tumaini kasalile
Mkala nzuri
Mwanahamisi
inabidi walipwe fidia
aisha
Duuh sio powa kabisa kupelekana huko
felister
alipwe haki zake jamani
Khadija
Asante kwa taarifa#meridianbettz
Issa
Wanapaswa wasimamie kwenye haki yao
Saupha mohamed
Inabidi alipwe
Sabrina
Wangemlipa tu haki yake
Amiri Kayera
Ujanja mwing walipe
farida ahmadi
Nouma Sana hiyo
Rose kapinga
Sheria ipo ivyo ukivunja mkataba inabidi wamlipe sasa mbona Barcelona wanaleta janja ya nyani!!
Fatuma kasomo
Asante kwataarifa@meridianbet
Mariam mtandama
Makala mazur
Tatu
Sheria itafuata mkondo wake
Gabriel
Jambo la aibu kubwa sana kwa club kubwa Kama Barcelona
Janeflora malisa
🔥
Povel
Duh majAnga kwl
Neema
Angelipwa tu wasifikie hatua mbaya
Latifa juma mohamed
Daah hatar
David Pere
Haki yake setien kupata kile anachostahili kama wao klabu ndio waliovunja mkataba huo
warda
usipotimiza mashart lazima ushtakiwe
Fatina mfigi
Duuuh
Salma ngende
Sheria ifatwe
Shan
Safi kudai haki yake
Samiah
Duuh