Kocha Pep Guardiola, 49, amesema atatia saini mkataba mpya kambini mwa Manchester City iwapo atahisi “anastahiki” kufanya hivyo badala ya kupewa mkataba huo.
Kandarasi ya sasa kati ya mkufunzi huyo raia wa Uhispania na Man-City unatarajiwa kutamatika rasmi mwishoni mwa msimu huu na ni matamanio ya usimamizi wa miamba hao kumshuhudia Guardiola akirefusha muda wake pale Etihad.
Guardiola anaanza msimu wake wa tano kambini mwa Man-City mnamo Septemba 21 atakapowaongoza waajiri wake kuvaana na Wolves katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) katika uwanja wa Molineux.

Hiki ndicho kipindi kirefu zaidi kwa Guardiola kuhudumu katika kikosi kimoja baada ya kudhibiti mikoba ya Barcelona (2008-12) na Bayern Munich (2013-16).
“Ningependa sana kusalia hapa Etihad kuwanoa Man-City. Nimeishia kuyapenda mazingira ya hapa ila nahitaji kustahili kupewa kandarasi mpya.
Man-City wamefaulu kujivunia mengi katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita na ni lazima tuendeleze rekodi hiyo,” akasema Guardiola ambaye ni mchezaji wa zamani wa Barcelona.
Kwa mujibu wa Guardiola, hakuna yeyote kati ya Mwenyekiti Khaldoon Al Mubarak au Afisa Mkuu Mtendaji Ferran Soriano ambaye amewahi kumzungumzia kuhusu mkataba mpya.
Ingawa anahisi kwamba matarajio kutoka kwake ni ya kiwango cha juu hasa baada ya kusuasua kwao muhula uliopita ambao ulishuhudia tofauti ya alama 18 kati yao na mabingwa Liverpool.

Man-City pia walibanduliwa na Olympique Lyon ya Ufaransa kwenye robo-fainali za Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) na hilo likawapa Bayern kibarua rahisi cha kuifunga Lyon (3-0) kwenye nusu-fainali na hatimaye kutwaa ufalme baada ya kuwapiga Paris Saint-Germain (PSG) 1-0 kwenye fainali jijini Lisbon, Ureno.
“Wasimamizi wa Man-City hawakunipa masharti: kwamba lazima utimize haya au yale ndipo uongezewe mkataba. Waliniambia niongoze kikosi kucheza soka nzuri,” akatanguliza.
“Lakini najua hadhi ya klabu hii pamoja na matamanio yao. Matarajio kutoka kwa mashabiki pia ni ya kiwango cha juu. Lazima turejelee kushinda mataji,” akaongeza.
FURAHIA KASINO YA MTANDAONI
Tembelea ardhi ya maajabu ushangazwe na mengi ikiwa ni pamoja na urahisi wa kujipatia utajiri kupitia Kasino ya Meridianbet.


Shan
Guadiola anahitaj atafute maisha mengine asiharibu cv yake kwa kufukuzwa
Khadija
Muda wako ukifika utasain tuu
Hopemwaikuka
Uamuz ni wako
Issa
Guadiola kama anahtaj kusepa na swala la champion league kama limekuwa kipengele sana hapo city pamoja na mabosi kumpatia fedha za kusajili wachezaj awatakao
felister
uamuzi anao yeye mwenyewe
Sabrina
Namkubali sana Pep Giadiola
aisha
Kweli guardiola haina maana kukufukuza muda ukifika itakua hivyo
Tumaini kasalile
Mimi nadhani anataka fedha iongezeke
Aziza mushi
Maamuzi anayo yeye
Theckla
Uwamuzi mzuri
Ernest
Pep no kocha Bora sana katika kipindi hiki, Nadhani kama mwenyewe pia atapenda kuwepo Mancity Mud mrefu nahisi hakuna kipingamizi
magdalena
guardiola aendelee tu kutulia apo city bado ana msaada mkubwa sana
Elika
Mimi nadhani angetafuta chaka sehemu nyingine
Dorophina
Guardiola ni bora asalie man city
Lydia Emmanuel Magoti
Yupo sahii Guardiola anacho kisema
Tatu
Maamuzi anayo mwenyewe
Caroline
Mbona Kama anasua sua kusaini huo mkataba
Angelina
Muda ukifika tutajua kama atasain
Zeiyana
Guadiola hana mengi ya kuifanyia man city kuondoka kwa sasa hitakua wakati mgumu clabuni pale
Sadick
Anapima upepo kwanza kuona mwelekeo wa timu kabla ya kusaini tena ama atafuta changamoto mpya#meridianbettz
Antony Luseno
Kama ni heshima kashapata nchi mbali mbali kwa sasa inamfaa atulie timu moja kwa muda mrefu
Neema
Maamuzi yako kwake muhusikaa
Amani
Me Kama naona awezi salia
Salma ngende
Hapo anaangalia mkwanja
Gabriel
kipengele sana hapo city pamoja na mabosi kumpatia fedha za kusajili wachezaj Guadiola hana mengi ya kuifanyia man city kuondoka kwa sasa hitakua wakati mgumu clabuni pale
Faraja molell
Nakukubali sana
Venerose
Guardiola anatakiwa atafute maisha mengine
Janeflora malisa
Uwamuz ni wake
Ester jackson
Kweli kocha Guardiola ameamua msimu huu hataki mchezo akawa lawama kwa kujitia kitazi mwenyewe safii sana neipenda hii
Rose kapinga
Vipi unakwama wapi!!
Saupha mohamed
Maamuzi yake
marry
afanye maamuz sahh
Frank P
Coach mwenye mahesabu
Sauda
Kila jambo na wakati wake
Latifa juma mohamed
Muda ukifika atasaini
Mwajumah
Uwamuzi anao yy mwenyew
Samiah
Uwamuzi anao yy
David Pere
Guadiola kama anahtaj kusepa na swala la champion league kama limekuwa kipengele sana hapo city pamoja na mabosi kumpatia fedha za kusajili wachezaj awatakao