Goli kipa namba 1 wa Man United na timu ya taifa ya Hispania – David De Gea, amenukuliwa akisisitiza kujisikia vizuri zaidi sasa hivi kupambanishwa na Dean Hernderson.
De Gea amekuwa na wakati mgumu kwa siku za karibuni kwa kile kinachoonekana ni kushuka kiwango. Amekuwa akifanya makosa ambayo kwa golikipa wa kiwango chake, hakupaswa kuyafanya.
Kuibuka kwa Dean Henderson ambaye alikuwa Shefield United kwa mkopo wa misimu miwili na sasa amerejea kwenye kikosi cha Man United. Kunaonekana kama ni kuhatarisha nafasi ya De Gea kwenye kikosi hicho.
Pamoja na yote anayoyapitia David, kocha Ole Gunnar Solskjaer amekuwa akimkingia kifua na kusisitiza nafasi ya kipa huyo haitobadilika licha ya kurejea kwa Henderson ambaye yupo kwenye kiwango thabiti kwa sasa.

Akizungumza na ukurasa rasmi wa Man United, De Gea amesema ” ninajisikia vizuri sana na ninajiamini zaidi kwa sasa, hiki ndio kitu cha muhimu kwangu. Sasa ni muda wa kurejea kwenye ushindi na kubeba mataji. Hili ni muhimu zaidi kwetu.
“Inapendeza kuwepo kwenye mazoezi kila siku, ninafurahia kufanya mazoezi na walimu wetu pamoja na magolikipa wenzangu. Kila siku tunajifunza wenyewe kwa wenyewe na kujitahidi kuimarishana kwa pamoja.
“Tunatakiwa kuwe kwenye kiwango hiki kila siku na kuwaonesha wachezaji wenzetu kama idara ya golikipa tupo vizuri kwa asilimia 100, sasa tunataka mataji.”
Man United watakuwa uwanjani leo mchana kupambana na Brighton Albion kwenye mchezo wa 2 wa EPL baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Crystal Palace.
FURAHIA KASINO YA MTANDAONI
Tembelea ardhi ya maajabu ushangazwe na mengi ikiwa ni pamoja na urahisi wa kujipatia utajiri kupitia Kasino ya Meridianbet.


Lydia Emmanuel Magoti
Duu De Gea angalie asije kushuka zaidi nafasi yake apewe mwengine na Yeye anzee kusugua benchi
Tatu
De gea alijisahau kwenye uchezaji wake mpaka kushuka kiwango kwanza alijiamini sana alijiona yupo peke yake akuna wa kushindanishwa nae
Adelta
Ni vizuri tuone Nani zaidi
Antony Luseno
Siku si nyingi Dean ataweza kumpiku De gea endapo kama kiwango chake kitaendelea kutoridhisha
Sadick
De Gea ameshuka kiwango ni muda sasa kumupisha Dean kama golikipa namba moja wa Man U#meridianbettz
aisha
Mmmh acha tuone nani atakua mkali zaidi
Shafii
Atakae kua kwenye kiwango bora ndiye atakaye kua kwenye kikosi cha Kwanza.
Saupha mohamed
Dean sasaiv yupo vizuri
farida ahmadi
De gea ni kipa mzuri Sana
Mwajumah
Kazi itakuwepo apo ila acha tuone nan atakua zaidi ya mwenzie
Khadija
Tuache maneno manone kila mtu anataka kujiona yy bola kwa mwenzie
Fatina
Mmmh ngoja tuone
Marry Mushi
kila kitu ni maamuz cha msngi ni kuonyesha bidii zaid
Agness
Mmmm hii Ni Vita sasa tunasubiri mshindi
Venerose
Nasubir kuona nani atakuwa zaidi ya mwingine
Zeiyana
Man Chester united hawawezi kusahau humuhimu wa de gea clabuni hapo na ndio maana wameamua kumpa nafasi yengine tena
Shani
Dean bado sana kufikia levo za de gea
Caroline
De Gea ameshuka kiwango
Hopemwaikuka
Haya kaendelee kuonyesha maajab yako
Elika
Dah sijui nani atakuwa mkali hapo
Hidaya
Pambano la nguvu
Amiri Kayera
De gea kiwango chake kimeshuk san
Nasra
Ngoja tuone kiwango chake
Gabriel
De gea n kipa mzur ila anajisahau sana
lombo
saf
Rehema
Ngoja tuone
Ernest
De Gea haba ubaya shida ipo kwenye backline ya Man U
Flomena
Good De Gea go go go
Samiah
Ngoja tuone
Neema
Ni mda sasa wakuonyesha juhudii kali tuone nani kamzidi mwenzake
Latifa juma mohamed
Duu De Gea angalie asije kushuka zaidi nafasi yake
David Pere
Man Chester united hawawezi kusahau humuhimu wa de gea clabuni hapo na ndio maana wameamua kumpa nafasi yengine tena
felister
changamoto nyengine nyengine kwa de gea
Rose kapinga
Juhudi zinaitajika apo!!!
Sabrina
De gea fundi jaman
magdalena
de gea ni goal keeper mzuri ila kiwango chake chaonekana kushuka kila kukicha anatuvunja sana moyo sisi mashabiki wa united
Dorophina
De gea ni kipamzuri sana anajua kucheza na nyavu
Povel
Ngoj tuone vita hiii itakwishaje