Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Neymar da Silva Santos Junior ana deni la €34.6 million la mamlaka ya kutoza ushuru nchini Uhispania.
Tovuti ya Get French News imesema Jumatano kuwa mamlaka hiyo imetoa orodha ya watu binafsi na kampuni inazowadai fedha.
“Katika orodha hiyo, kuna mshambuliaji wa Brazil na PSG, Neymar, ambaye anafaa kulipa ushuru wa €34.6 million (Yuro 34.6 milioni),” tovuti hiyo imesema.

Kiasi hicho cha fedha, tovuti hiyo imefichua, kinatoshana na ushuru ambao Neymar hajalipa unaotokana na marupurupu aliyopokea kutoka kwa waajiri wake wa zamani Barcelona alipokuwa ameongeza kandarasi yake uwanjani Camp Nou mwaka 2016 kabla ya kuhamia mjini Paris nchini Ufaransa mwaka 2017 akiwa hajakamilisha kandarasi yake.
Neymar alijiunga na PSG baada ya mawakili wake kulipa Barcelona €222 million mnamo Agosti 3, 2017. Kiasi hicho kilikuwa ada ya kumruhusu aondoke Barca iliyokuwa imeweka kipengee cha kumzuia kuondoka kabla ya kiasi hicho kutolewa katika kandarasi yake.
Uhamisho wa kutoka Barca hadi PSG unasalia kuwa ghali kuwahi kushuhudiwa katika historia ya soka. Barca walimshtaki Neymar hapo Agosti 27 mwaka 2017 ikitaka arejeshe marupurupu ya kusaini kandarasi mpya uwanjani Camp Nou, fidia ya €6.7 million pamoja na nyongeza ya asilimia 10 ya malimbikizi.

Mwaka 2016, mahakama moja jijini Rio de Janeiro nchini Brazil pia ilipata hatia ya kulaghai mamlaka ya ushuru nchini mwake ili kujinufaisha. Alitozwa faini ambayo ilikuwa ushuru, faida na faini.
Inasemekana wakati huo Neymar alikuwa amekwepa kulipia ushuru mapato yake kwenye kandarasi zake kati ya mwaka 2011 na 2013 ambazo zilikuwa kutoka klabu yake ya zamani Santos nchini Brazil, Barcelona pamoja na kampuni ya vifaa vya michezo, Nike.
Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!
Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!


Adelta
Mashabiki tunashukuru kwa makala nzuri
Dorophina
Mchezaji mkubwa kama Neymar sio vizuri kuwa na skendo kama hizo
magdalena
duh sasa izo ni balaa sheria kali sana
Elika
Dah kwanini tena Neymar nae..afanye mchakato tuu alipe
Ester mmakasa
Si majanga hayo kwa neyma inabidi alipe ili ajiepushe na hayo malawama.
Fatina mfigi
Duuh majanga hayo kwa neymar bora alipe tyu
Ernest
Hizi kashfa za kimagumashi kwa Neymar kila mwaka, Vyombo husika vinatakiwa viwe makini maana inaonekana kama kama wanapenda kuzusha mambo ili kufuna mkwanja
Lydia Emmanuel Magoti
Duu hiyo Kali kwaiyo Sheria imefata mkondo wake kwaiyo Neymar anatakiwa kulipa deni kwamchezaji mkubwa Kama Neymar kuzalilishwa Kama ivyo sio poa duu Atari hiyo
Sauda
Neymar alipe tu ushuru ili awe huru.
Zeiyana
Staa kama neymar kitu kidogo tu hicho ukiangalia juzi tu kapata ubarozi kwenye kamponi kubwa litakwisha tu hilo
Caroline
Iyo hela ni ndogo Sana kwa Neymar
Mwanahamisi
Sasa hivyo ni balaa
Mwajumah
Duuh majanga ayo kwa neymar
Venerose
Alipe tu ili afanye kazi kwa uhuru
Nasra
Hatarii sana
Khadija
Duh!!imekuwaje sasa hela zote
Janeflora malisa
Asnt kwa taarif
Tatu
Majanga mengine haya
Rehema
Asante kwa taarifa
Hopemwaikuka
Raha ya den kulipa
Neema
Ni afadhalii alipe deni ili awe huru
Zuhura omary kindamba
Pole yake ila dawa ya deni kulipa
Saupha mohamed
Duuuu majanga
Shani
Swala hili linatakiw likomeshw kwakua wachezaji wamekua wanasumbua juu ya kodi hili limetokea kwa mastaa kadhaa
Povel
Skendo za madeni ya malimbikizo ya kodi imekuwah jambo la skendo kila mwaka natumain ifike wakati mamlaka husika wafanye kazi kwa ufasaha ilikupisha malamiko ya kila mwaka Kama haya
lombo
duuh
Issa
Imekua tabia kwa mastaa kukwepa kodi inabid mamlaka husika zisimamie hili
Sabrina
Duh alipe tu hana jinsi
Angelina
Dawa ya deni kulipa
Amiri Kayera
Dah npesa nyingi San anadaiwa
Latifa juma mohamed
Neymer alipe tu , ili awe huru.
Gabriel
Vyombo husika vinatakiwa viwe makini maana inaonekana kama kama wanapenda kuzusha
Samiah
Duuh