Tottenham imefikia makubaliano ya kumsaini mshambuliaji Carlos Vinicius kwa mkopo akitokea klabu ya Benfica mpaka mwisho wa msimu, miamba hao wa Ureno walitangaza siku ya Alhamisi.
Dau la Euro milioni 3 (£2.7m) katika dili hiyo kwa Carlos Vinicius pia inajumuisha kipengele cha kumnunua kwa kitita cha £41m sawa na Euro milioni 45 ingawa kiasi cha mkopo kinachotakiwa kulipwa kinaweza kupunguzwa.
Tottenham walikata tamaa ya kumsaini msaidizi wa Harry Kane, baada ya hapo nyuma kuhusishwa na kumsaini mchezaji wa Napoli Arkadiusz Milik na nahodha wa Torino Andrea Belotti.

Timu ya Jose Mourinho kwa sasa imemgeukia mchezaji wa Kibrazil Carlos Vinicius, ambaye alijiunga na Benfica akitokea ligi ya Serie A katika klabu ya Napoli mwaka uliyopita.
Carlos Vinicius alifunga magoli 18 katika michezo 32 ya Primeira Liga msimu uliyopita, lakini pia alikuwa amefungaa jumla ya magoli 22 kataika mashindano yote.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alimaliza msimu wa 2019-20 katika Primeira Liga, wakati Benfica ikimaliza nafasi ya pili nyuma ya mahasimu wao Porto na kuwa mfungaji bora akiwa na mchezaji mwenzake Pizzi na mchezaji wa Rio Ave Mehdi Taremi.
Hali ya kuwa katika sintofahamu kuhusu hatima yake, Carlos Vinicius amecheza dakika 18 pekee msimu huu mpya na kocha mkuu Jorge Jesus amewapa nafasi zaidi wawili Darwin Nunez na Luca Waldschmidt.
Tottenham imefuzu kucheza Europa League katika hatua ya makundi kwa kuichapa 7-2 timu ya Maccabi Haifa jijini London siku ya Alhamisi wakati pia wapo nafasi ya nane katika msimamo wa Premier League wakiwa wamekusanya alama 5.
Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!
Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!


Dorophina
Kila lakheri Carlos katika majukumu yako spurs
Adelta
Carlos piga Kazi kikubwa maslai tu
Tatu
Corlos huko ndio panamfaa
magdalena
carlos bora ameenda ata uko kwa mkopo maana kipaji chake naona kama kilianza kusinzia
Elika
Safi kijana kambi popote
Ester mmakasa
Sio mbaya ilimradi mkono unaenda kinywani.
Fatina mfingi
Kambi popote kijan kapige kazi!!
Lydia Emmanuel Magoti
Kila la kheri Carlos kwenye krabu yako mpya utakayo Anzanayo
Ernest
Naona Mourinho anazidi kujizatiti, huenda Carlos Vinicius akamsadia Mourinho plan A ya Kane ikifeli
Sauda
Maisha popote, piga kaz
Caroline
Mourinho ananoa kikosi
Zeiyana
Carlos yupo vizuri ndio maana kila clabu yingi zimekua zikimtolea macho
Mwajumah
Safi sana kambi popote tu
Venerose
Carlos yupo vinzur
Nasra
Carlos yupo fit
Khadija
Kapige kezi kijana
Janeflora malisa
Asnt kwa taarif
Hopemwaikuka
Sawa tu kulko kukosa kabsa
Rehema
Good news 👍
aisha
Carlos yuko vizuri sana
Neema
Maisha popotee
Zuhura omary kindamba
Carlos piga kazi kambi kokote
Saupha mohamed
Siyo mbaya
Shani
Tottenham ikimtumia vinicius atawasaidia
Sana
Povel
Naona Mourinho anatafut mbadala sahihi wa endapo Kama KANE atapata injured hawe plan B
Issa
Totenham wanjitahid kuiweka timu sawa ila mournho ajitahid kwa usajili
Sabrina
Kapige kazi
Angelina
Khila la kheri
Amiri Kayera
Mchezaji mzur
Latifa juma mohamed
Kazikazi piga kazi kambi popote.
Gabriel
Carlos Vinicius akamsadia Mourinho
Samiah
Gud